TAARIFA YA MKOA WA RUKWA YA
MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA UHURU (DISEMBA 1961 HADI 2011).
1.0 UTANGULIZI.
Mkoa wa Rukwa upo Kusini Magharibi mwa Tanzania. Ulianzishwa mwaka 1974
kwa kumega Wilaya ya Sumbawanga kutoka Mkoa wa Mbeya na Wilaya ya Mpanda kutoka
sehemu ya Mkoa wa Tabora. Mwaka 1979 Wilaya ya Nkasi ilianzishwa, hivyo Mkoa
ukawa na Wilaya tatu Tarafa 21, Kata 79 na Vijiji 372. Mkoa una eneo la km. za
mraba 75,250. Kati ya hizo km. za mraba 68,645 ni za nchi kavu na km. za mraba
6,605 ni za maji.
Kulingana na Sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 1988 mkoa wa
Rukwa ulikuwa na jumla ya watu 703,050 ambalo ni ongezeko la 4.5%, lakini sensa ya watu na makazi iliyofanyika Agosti, 2002 wakazi wa mkoa wa
Rukwa walikuwa wameongezeka hadi 1,136,354. Mwaka 2011 Mkoa unakisiwa kuwa na
wakazi 1, 558,200 ambalo ni ongezeko la asilimia 3.6% kwa mwaka. Mkoa huu unapakana na Mikoa ya Tabora, Kigoma
na Mbeya. Aidha unapakana na nchi za Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo.
UMBILE LA MKOA WA RUKWA KWA KIFUPI.
Kabla ya
mabadiliko yaliyofanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi
June 2010, Mkoa ulikuwa na Wilaya 3, Majimbo 7 ya Uchaguzi, Halmashauri 5,
Tarafa 21, Kata 88, Vijiji 379 na Mitaa 134.
HALI YA ULINZI NA USALAMA.
Kwa kipindi
cha Miaka 50 hali ya Ulinzi na Usalama katika mkoa ni shwari na ya kuridhishwa
kwa kiasi kikubwa. Mtukio machache ya uhalifu yanayojitokeza yameendelea
kushughulikiwa na kudhibitiwa na Kamati za Ulinza na Usalama za kila Wilaya kwa
kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.
Matukio haya
ni katika maeneo ya Mwambao wa Ziwa Tanganyika. Kwa namna ya pekee tunashukuru sana
uwepo wa vikosi viteule vya Jeshi la wananchi katika Vijiji vya Kirando,
Kasanga na Ikola ambavyo vinafanya kazi nzuri sana ambayo imesaidia kupunguza
matukio ya uvamizi katika Mwambao wa Ziwa Tanganyika. Tunashukuru pia kwa
jitihada za JWTZ kuonyesha nia ya kujenga kikosi cha JWTZ Wilaya ya Nkasi
wananchi wa Mkoa wa Rukwa wanaimani kuwa uwepo wa kikosi utaimarisha zaidi
Ulinzi na Usalama wa maeneo mbalimbali ya Mkoa.
HALI YA KISIASA
Baada ya Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961
mkoa ulikuwa unaongozwa na chama kimoja cha siasa kilichojulikana kwa jina la
TANU, Mwaka 1977 chama hiki kiliungana na chama cha ASP- cha Zanzibar na kuunda
Chama Cha Mapinduzi. Mwaka 1992 ulianzishwa
mfumo wa vyama vingi nchini mpaka mwaka 2011 vyama vya siasa vilivyopo mkoani
Rukwa ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia (DP), NCCR-MAGEUZI,
UDP na TLP.
SHUGHULI ZA
KIUCHUMI NA PATO LA MKOA WA RUKWA KWA KIFUPI.
Kiuchumi, wakazi wa mkoa wa Rukwa wanajishughulisha
na ufugaji, kilimo cha mazao ya chakula na biashara, sekta ya utalii, madini,
uvuvi, viwanda vidogo pamoja na biashara
ndogondogo. Pato la Mkoa limekuwa likiongezeka mwaka hadi mwaka, kutoka kiwango
cha 3.5% mwaka 1999 hadi kufikia 3.7% mwaka 2004. Kuhusu pato la mwananchi,
nalo pia limekuwa likiongezeka kutoka shilingi 239,943 mwaka 1999 hadi kufika Shilingi
369,993 mwaka 2004, na takwimu za mwisho za mwaka 2007 wastani wa pato la Mkoa
ulikadiriwa kuwa Shilingi 486,832 kwa mwaka.
DIRA
YA MKOA WA RUKWA.
Dira ya Mkoa ni “kuhakikisha
kuwa huduma zote muhimu zinatolewa kwa wadau wote kwa wakati na kwa kiwango cha
juu na kinachokubalika siku zote kwa ajili ya maisha bora na mazuri ili kuweza
kuondokana na umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2025”.
VIPAUMBELE VYA MKOA.
Katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi na MKUKUTA na kwa kuzingatia
Jiografia, majukumu na malengo ya Mkoa yamejikita katika kutekeleza vipaumbele
vifuatavyo: Kuboresha Miundombinu, Kilimo, Elimu, Maendeleo ya Watumishi,
Mazingira, Maji, Huduma za Afya, Mapambano dhidi ya UKIMWI na kuhamasisha
uanzishaji wa SACCOS.
MAFANIKIO YA
MKOA WA RUKWA KWA MUDA WA MIAKA 50 YA UHURU.
Katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru Mkoa wa Rukwa umeendelea
kutekeleza majukumu mbalimbali katika kupambana na Umaskini, Ujinga na Maradhi.
Kwa kipindi chote cha Miaka 50 ya Uhuru Mkoa wa Rukwa umepata mafanikio makubwa
ya Maendeleo katika nyanja za Kiuchumi, Kijamii, na Kisiasa. Baadhi ya
Mafanikio hayo ni kuanzishwa kwa Mkoa Mpya wa Rukwa mwaka 1974, kuanzishwa kwa
Wilaya tatu za Mpanda, Nkasi na Sumbawanga pamoja na uanzishwaji wa Halmashauri
tano ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Mpanda, Sumbawanga na
Halmashauri ya Mji Mpanda na Manispaa ya Sumbawanga pia mwezi Juni 2010 Mhe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitangaza kuanzishwa kwa Mkoa Mpya wa
Katavi na Wilaya ya Mlele.
2.0 MAFANIKIO YA MKOA YA MIAKA 50 YA UHURU KWA KILA
SEKTA.
Mkoa wa Rukwa katika kipindi
cha Miaka 50 ya Uhuru wa
·
Wakati
mkoa wa Rukwa unaanzishwa mwaka 1974 hapakuwepo na mwongozo mahsusi
ulioandaliwa na mkoa kwa ajili ya kuendeleza Sekta ya Kilimo lakini mwaka 2008
Mkoa wa Rukwa umefanikiwa kubuni Mwongozo (mpango) wake unaojulikana
·
Kuanzia
mwaka 1961 hadi mwaka 2000 bajeti ya maendeleo ya Sekta ya Kilimo iliyokuwa
inatolewa ilikuwa kidogo isiyoweza kuendeleza na kuinua sekta ya Kilimo lakini
katika bajeti ya mwaka 2010/11 bajeti ya sekta ya kilimo imeongezeka kufikia Sh
7,501,889,895/=.
·
Eneo
linalolimwa mazao ya biashara limeongezeka kutoka hekta 2,188 mwaka 1961 hadi
hekta 109,388.7 mwaka 2011.
·
Uzalishaji
wa mazao mbalimbali ya chakula umeongezeka kutoka tani 39,397 mwaka 1961 hadi
1,969,873.8 mwaka 2010.
·
Uzalishaji
wa mazao ya biashara umeongezeka kutoka tani 5,381 mwaka 1961 hadi tani
269,057.1 mwaka 2010.
·
Matumizi
ya mbolea yameongezeka kutoka tani 372.9 mwaka 1961 hadi tani 18,644.5 mwaka
2011.
·
Mbolea
ya ruzuku imeongezeka kutoka tani 268 mwaka 2005 hadi tani 13,400 mwaka 2011.
·
Matumizi
ya wanyamakazi (maksai) katika kilimo yameongezeka kutoka 5% mwaka 1961 hadi
70% mwaka 2011.
·
Matumizi
ya mbegu bora yameongezeka kutoka tani 81 mwaka 2005 hadi tani 4,025.5 mwaka
2011ukilinganisha na hali ilivyokuwa wakati mkoa unaanza ambapo wakulima
walitumia mbegu asilia tu.
·
Matumizi
ya matrekta madogo yameongezeka toka 0 mwaka 1961 hadi 225 mwaka 2011.
·
Matumizi
ya matrekta makubwa yameongezeka kutoka matrekta 1 mwaka 1961 hadi matrekta 85 mwaka
2011.
·
Kilimo
cha umwagiliaji kimeongezeka kutoka hekta 543 mwaka 2000 hadi hekta 27,136
mwaka 2011 ukilinganisha na hali ilivyokuwa wakati mkoa unaanza ambapo wakulima
walilima kwa kutegemea majira ya mvua tu.
2.1.2
MIFUGO
MAFANIKIO
– 1961 HADI 2011.
·
Majosho
yanayofanya kazi yameongezeka kutoka 0 mwaka 1961 hadi 36 mwaka 2011.
·
Wataalam
wa uhamilishaji (Artificial Insemination) wameongezeka kutoka 0 mwaka 1961 hadi
18 mwaka 2011 (wakijumuishwa wafugaji 6).
·
Madume
bora yameongezeka kutoka 4 kwa mwaka 1961 hadi 210 mwaka 2011.
·
Idadi
ya ng’ombe waliohamilishwa imeongezeka kutoka 7 mwaka 1961 hadi 363 mwaka 2011.
·
Dawa
za kuogesha mifugo zenye ruzuku ya Serikali zimeongezeka kutoka lita 0 mwaka 2006 hadi lita 39,426.75 mwaka 2011.
Ambapo mwanzo serikali haikuwa na mpango wa kutoa ruzuku kwa ajili pembejeo za
kilimo.
·
Elimu
kupitia mashamba darasa ya ufugaji imeongezeka kutoka 0 mwaka 1961 hadi
mashamba darasa 62 mwaka 2011.
·
Malambo
ya maji ya kunywesha mifugo yameongezeka kutoka 0 mwaka 1961 hadi 2 yaliyoko katika
hatua za ujenzi mwaka 2011.
·
Idadi
ya wafugaji waliopata mafunzo ya ufugaji bora imeongezeka kutoka 0 mwaka 1961
hadi 8411 mwaka 2011.
·
Mbuzi
wa Maziwa wameongezeka kutoka 16 mwaka 1961 hadi 791 mwaka 2011.
·
Ng’ombe
wa maziwa wameongezeka kutoka 136 mwaka 1961 hadi 6,797 mwaka 2011.
·
Utengaji
wa maeneo ya malisho ya mifugo umeongezeka kutoka vijiji 0 mwaka 1961 hadi
vijiji 73 mwaka 2011.
2.1.3 UVUVI
MAFANIKIO – 1961 HADI
2011.
·
Matumizi ya zana bora za uvuvi yameongezeka kutoka
injini za boati 20 mwaka 1961
hadi injini za boti 1024 mwaka 2011.
·
Katika kuwasaidia wavuvi kutumia maarifa ya kisasa
ya uvuvi, waliopatiwa elimu ni 0 mwaka 1961
hadi 15,016 mwaka 2011.
·
Katika jitihada za kupambana na uvuvi haramu idadi
ya zana haramu zilizokamatwa na kuteketezwa zimeongezeka kutoka zana haramu 0
mwaka 1961
hadi 1484 mwaka 2011.
·
Mkoa umeunda kikosi kazi cha watu 12 kwa ajili ya kuinua
sekta ya uvuvi mwaka 2011.
·
Ufugaji wa samaki umehamasishwa kwa kuanzisha
mabwawa ya kufugia samaki 0 mwaka 1961
hadi 700 mwaka 2011.
2.1.4 USHIRIKA /SACCOS.
MAFANIKIO
– 1961 HADI 2011.
·
Idadi
ya vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo (SACCOS) imeongezeka kutoka vyama 0 mwaka 1961 hadi 105 mwaka 2011.
·
Mtaji umeongezeka kutoka 0 mwaka 1961 hadi
kufikia sh. 2,301,203,127/= mwaka 2011.
·
Aina
nyingine za vyama vya ushirika vimeongezeka kutoka 0 mwaka 1961 hadi 29 mwaka
2011 ikiwa ni ongezeko la asilimia 100 na mtaji wa vyama hivi umefikia sh. 95,664,500/=.
·
Katika
kipindi cha miaka 50 ya Uhuru SACCOS za Rukwa zimepata jumla ya mikopo yenye
thamani ya Sh. 6,101,992,400/= na jumla ya Sh. 3,572,981,541/= zimerejeshwa
sawa na asilimia 59.4 ya mikopo iliyotolewa.
·
Tumekwisha
anza mchakato wa kuanzisha Benki ya wananchi wa Mkoa wa Rukwa (Rukwa Community
Bank ‘RCB’).
2.1.5
MAZINGIRA.
MAFANIKIO – 1961 HADI 2011.
·
Uhifadhi
wa vyanzo vya maji umeongezeka kutoka vyanzo 0 mwaka 1961 hadi 86 mwaka 2011.
·
Matumizi
ya mizinga ya kisasa ya nyuki yameongezeka kutoka mizinga 0 mwaka 1961 hadi 5566 mwaka 2011.
·
Mipaka
ya vijiji vyote 379 (100%) vya Mkoa imeshapimwa; vijiji 44 vimeandaa matumizi
bora ya ardhi.
·
Hadi
mwaka 2011 jumla ya miti 19,069,983 ilikuwa imepandwa.
·
Halmashauri
zote zimetunga sheria ndogo za kudhibiti mazingira.
·
Mkoa
umezuia uingizaji wa mifugo mipya Mkoani.
3.1 ELIMU
(i) ELIMU YA AWALI:
Madarasa ya elimu
ya awali yameongezeka kutoka 0 mwaka 1961 hadi 844 (2011).
(ii) ELIMU YA MSINGI:
·
Asilimia
ya uandikishaji darasa la kwanza imeongezeka kutoka chini ya asilimia 100 mwaka
1961 hadi asilimia 123.84 (2011).
·
Idadi
ya Wanafunzi darasa la I – VII imeongezeka kutoka 5,968 (mwaka 1961 hadi
298,408 (2011).
·
Idadi
ya shule za Msingi imeongezeka kutoka 10 mwaka 1961 hadi 508 (2011) ongezeko 5,080%
zikiwemo shule 2 zisizo za serikali.
·
Idadi
ya walimu imeongezeka kutoka 97 mwaka 1961 hadi 4840 (2011).
·
Idadi
ya nyumba za walimu imeongezeka kutoka 42 mwaka 1961 hadi 2089 (2011).
·
Uwiano
wa Kitabu kwa mwanafunzi (Book Pupil Ratio) umepungua na kufikia 1:3 na 1:4
hivi sasa.
·
Idadi
ya wanafunzi wanaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza imeongezeka kutoka 73 mwaka
1961 hadi 3,672 (2011
(iii) ELIMU YA SEKONDARI:
·
Idadi
ya shule za Sekondari za Serikali imeongezeka kutoka 0 mwaka 1961 hadi 99 mwaka
2011.
·
Idadi
ya shule zisizo za Serikali imeongezeka kutoka 0 mwaka 1961 hadi 15 mwaka 2011.
·
Shule
za Sekondari za Serikali zenye “A Level” zimeongezeka kutoka 0 mwaka 1961 hadi
8 mwaka 2011.
·
Shule
za Sekondari zisizo za Serikali zenye “A Level” zimeongezeka kutoka 0 mwaka 1961
hadi 4 mwaka 2011.
·
Idadi
ya wanafunzi imeongezeka kutoka 734 mwaka 1961 hadi 36,706 mwaka 2011.
·
Idadi
ya walimu imeongezeka kutoka 20 mwaka 1961 hadi 995 (2011).
·
Hivi
sasa Kata 86 kati ya 88 sawa na asilimia 97.7 zina shule za sekondari.
(iv) ELIMU YA UALIMU:
Idadi ya Vyuo vya
Ualimu imeongezeka kutoka 0 mwaka 1961 hadi 2 (2011) ongezeko la 100% baada ya
kusajiliwa Chuo kisicho cha serikali cha Rukwa.
(v) ELIMU YA UFUNDI:
Mkoa unavyo vituo
vya Ufundi Stadi 6 katika Shule za Msingi na Vyuo vya Ufundi 3 vinavyotoa
mafunzo ya Ufundi katika fani za useremala, uashi, ufundi chuma, ufundi magari,
uchomeleaji, kompyuta na Sayansi Kimu.
(vi).
ELIMU YA JUU:
Mkoa unatawi la Chuo Kikuu
Huria cha Tanzania kilichoanzishwa mwaka 2003 mpaka mwaka 2011 kuna vituo
viwili vya Chuo hiki, kituo kimoja kipo Mpanda na kingine Sumbawanga.
3.2 AFYA:
MAFANIKIO – 1961 HADI 2011.
·
Zahanati zimeongezeka kutoka 4 mwaka 1961 hadi
224 mwaka 2011.
·
Vituo vya Afya vimeongezeka kutoka 0 mwaka 1961 hadi
34 mwaka 2011.
·
Hospitali zimeongezeka kutoka 1 mwaka 1961 hadi 4 mwaka 2011.
·
Mahudhurio ya kwanza chini ya wiki 16 ya mama
wajawazito yameongezeka kutoka 0 mwaka 1961
hadi 54% (2011).
·
Kiwango cha mama wajawazito wanaojifungulia katika
vituo vya kutolea huduma za Afya na kuhudumiwa na wahudumu wenye mafunzo
kimeongezeka kutoka 0 mwaka 1961
hadi asilimia 58 (2010).
·
Vifo vya wazazi vimepungua kutoka 220/100,000 mpaka
134/100,000 (2010).
·
Utapiamlo mkali umepungua kutoka asilimia 8 hadi
asilimia 1 (2011).
·
Chanjo ya watoto chini ya mwaka mmoja imeendelea
kupata mafanikio
o
Polio (kutoka 93.2% hadi 101% (2011).
o
BCG (kutoka 92.7% hadi 102% (2011).
o
DPT HB3 (kutoka 90% hadi 92% (2011).
o
Measles (kutoka 95% hadi 122% (2011).
o
Pepopunda kwa wajawazito kutoka 80.5% hadi 109%
(2011).
·
Kumekuwepo na vituo vya kutolea tiba kwa wazee
katika Hospitali na vituo vya Afya mpaka kufikia Machi 2011 jumla ya wazee 14,
585 wamepata vitambulisho vya matibabu.
·
Vifo vya watoto wachanga (IMR) chini ya mwaka mmoja
vimepungua kutoka 106/1000 hadi 87/1000 mwaka 2011.
·
Vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimepungua
kutoka 175/1000 hadi 122/1000 mwaka 2011.
·
Serikali katika kuboresha huduma kwa watumishi wake
imeanza mpango wa kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa kujenga nyumba 10 za
watumishi katika kila Halmashauri. Mpango huu utasimamiwa na shirika la
Benjamin Mkapa kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI na Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii.
·
Mkoa una Chuo cha Wauguzi kinachoendeshwa na Kanisa
Katoliki Jimbo la Sumbawanga kilichopo Wilaya ya Nkasi Mjini Namanyere ambacho
kimetoa wahitimu wa kwanza 24 mwaka 2007, 42 mwaka 2008 na 84 mwaka 2009. Aidha, Mkoa una Chuo cha Waganga Wasaidizi
Vijijini (RMA) katika Manispaa ya Sumbawanga na unategemea kufungua kingine
katika Wilaya ya Mpanda mwishoni mwa mwaka huu wa 2011.
·
Umefanyika ukarabati wa Hospitali ya Mkoa kwa
kipindi cha miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2007/08 hadi 2009/10. Serikali
imetoa jumla ya Sh.1.8 bilioni kwa ajili ya ukarabati wa majengo 7, ujenzi wa
majengo 11 na ununuzi wa majenereta 2.
3.3 UKIMWI.
Tangu ugonjwa huu ugundulike Mkoani mwaka 1986, Serikali ya Mkoa
imechukua jitihada mbalimbali kukabiliana na tatizo
MAFANIKIO – 1986 HADI 2011.
·
Kiwango cha maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto mkoani kimepungua kutoka asilimia 6.7 hadi 4.9% mwaka 2011.
·
Katika huduma ya kuzuia maambukizi kutoka kwa mama
kwenda kwa mtoto (PMTCT) kuna ongezeko la vituo 66 vya kutolea huduma kutoka 38
hadi 104 mwaka 2011.
·
Vituo vya ushauri nasaha na upimaji wa hiari
vimeongezeka kutoka 0 hadi 85 mwaka 2011.
·
Idadi ya wateja waliojitokeza kupima kwa hiari
imeongezeka toka watu 782 hadi watu 240,000 mwaka 2011.
·
Asasi za kiraia 76 zinachangia kwa kiasi kikubwa
kutoa huduma kwa wateja wa UKIMWI hasa katika huduma za majumbani kwa
waathirika, watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu. Hadi sasa watoto
yatima na wanaoishi katika mazingira magumu zaidi ya 12,567 wametambuliwa na
kupewa huduma.
·
Vituo vya tiba ya kupunguza makali ya ukimwi
vimeongezeka kutoka 0 mwaka 1986
hadi 20 mwaka 2011.
·
Hali ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kwa sasa
kiwango kimeshuka kutoka asilimia 6 hadi 4.9% mwaka 2011 ikilinganishwa na
asilimia 5.8 ya wastani wa kitaifa.
Halmashauri inayoongoza ni Manispaa ya Sumbawanga kwa asilimia 6.5 na
Halmashauri yenye kiwango cha chini ni Nkasi yenye asilimia 3.1.
·
Wagonjwa wanaopata matibabu ya dawa za ARV
wameongezeka kutoka 0 mwaka 1986
hadi 6,175 mwaka 2011.
3.4 MAJI.
Katika
kipindi cha Miaka 50 ya Uhuru Mkoa umeendelea kusogeza huduma ya maji
3.5 MAFANIKIO –
MAJI.
Katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru mkoa umeendelea
kusogeza huduma ya maji
MAFANIKIO – 1961 HADI 2011.
·
Miradi ya maji ya kutega imeongezeka kutoka 0 kwa
kipindi cha mwaka 1961
hadi kufikia 36 mwaka 2011.
·
Visima virefu na vifupi vyenye pampu vinavyofanya
kazi vimeongezeka kutoka 22 kwa kipindi cha mwaka 1961 hadi 1079 mwaka 2011.
·
Idadi ya watu wanaopata huduma ya maji
·
Mradi wa maendeleo ya sekta ya maji umeanza
kutekelezwa ambapo katika Manispaa ya Sumbawanga kupitia Mamlaka ya Maji Safi
na Maji taka ya Sumbawanga mkandarasi amekwisha anza kazi ya ukarabati wa
mtandao wa maji na uchimbaji wa visima virefu unaendelea.
·
Halmashauri zetu zote Makandarasi washauri
wamekamilisha zoezi la uandaaji wa taarifa ambazo zitasaidia katika kutekeleza
mradi unaojulikana kwa jina la mradi wa vijiji 10 kwa kila Halmashauri.
Halmashauri zina kamati hai
na mifuko ya maji 273 yenye jumla ya shilingi 83,257,180.91/= hadi 2011.
·
Halmashauri
ya Mji Mpanda imejenga visima na matanki ya kusambazia maji kufikia wakazi
wapatao 2000 katika Kata ya Nsemulwa, Majengo na Kawajense.
3.6 MIUNDOMBINU.
Mkoa wa Rukwa una mtandao wa
barabara unaokadiriwa kuwa na kilomita 5,502.3. Mtandao wa barabara
unaohudumiwa na Wizara ya Miundombinu kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS)
Mkoani Rukwa una jumla ya kilomita 2,150 ambapo Barabara Kuu ni kilomita 887 na
barabara za Mkoa ni kilomita 1,263 mwaka 2011.
MAFANIKIO – 1961 HADI 2011.
Kwa muda wa Miaka 50 ya uhuru
Mkoa wa Rukwa haukuunganishwa na mikoa mingine kwa kiwango cha lami na hivyo
kufanya barabara za Mkoa kupitika kwa msimu. Lakini katika mwaka 2010/2011 Serikali
imesaini mikataba mbalimbali kwa ajili ya kutengeza barabara za mkoa kwa kiwango
cha lami mikataba hiyo ni:-
·
Mkataba
wa ujenzi wa Barabara ya Tunduma-Laela-Sumbawanga kwa kiwango cha lami ambapo
hivi sasa ujenzi unaendelea. Barabara hii imegawanywa katika sehemu tatu ili
kuharakisha ujenzi (Tunduma-Ikana km.64; Ikana-Laela km.64 na Laela-Sumbawanga
km.96.5).
·
Mkataba
wa ujenzi wa barabara ya Laela-Sumbawanga (96.5 km) kwa kiwango cha lami
ulisainiwa tarehe 29/04/2010 ambapo jina la Mkandarasi ni AARSLEEF-BAM International JV kutoka nchini
·
Mkataba
wa ujenzi wa barabara ya Ikana-Laela (64.2 km) kwa kiwango cha lami ulisainiwa
tarehe 17/09/2010 ambapo jina la Mkandarasi ni China New Era International Enginering Corporation kutoka nchini
·
Mkataba
wa ujenzi wa barabara ya Tunduma - Ikana (63.7 km) kwa kiwango cha lami
ulisainiwa tarehe 22/09/2010 ambapo jina la Mkandarasi ni Consolidated Contractors Group S.A (offshore)(CCC) kutoka nchini Ugriki na Egis BCEOM International
kutoka Ufaransa, barabara hii mpaka kukamilika itaghalimu Sh. 82.5 Bilion.
Maendeleo ya mradi hadi kufikia tarehe 31 Machi 2011 Mkandarasi alikuwa
anaendelea na maandalizi ya kuanza kazi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kambi
katika kijiji cha Chipaka Wilayani Mbozi.
·
Barabara
ya Sumbawanga-Chala-Kanazi (Namanyere) yenye urefu wa km.75 inajengwa na
Mkandarasi aitwaye Jiangxi
Geo-Engineering Group Corporation kwa gharama ya Shilingi 78,840,000,000/=,
mkataba huu ulisainiwa tarehe 15/06/2009. Maendeleo ya jumla ya mradi huu kufikia
31Machi 2011 yalikuwa 9.4% ya kazi zote zilizopangwa kuchelewa kwa malipo ya
Mkandarasi kumechangia utekelezaji wa mradi kuwa na kasi ndogo.
·
Barabara
ya Kanazi (Namanyere)-Kizi-Kibaoni yenye urefu wa km.76 inajengwa na Mkandarasi
aitwaye China Hunan Construction
Engineering Group Corporation kwa gharama ya Shilingi 82,840,000,000/=
mkataba ulisainiwa tarehe 15/07/2009, Maendeleo ya mradi huu hadi kufikia
tarehe 31 Machi 2011 yalikuwa 17% ya kazi zote zilizopangwa. Mkandarasi
anaendelea vizuri ingawa kuchelewa kwa malipo ya Mkandarasi kumeathiri kasi ya
utekelezaji wa mradi.
·
Mkataba
wa ujenzi wa Barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga yenye urefu wa km.112 kwa
kiwango cha lami ulisainiwa tarehe 7 Oktoba 2009. Mkandarasi aliyepewa kazi hii ni China Railway 15 Bureau Group Corporation
(CR15G) akishirikiana
·
Upembuzi
Yakinifu na Usanifu wa Kina (Feasibility Study and Detailed Engineering
Design) kwa barabara ya Mpanda-Uvinza-Kanyani (Kasulu) yenye urefu wa
km.252 unaendelea vizuri. Kazi ya upembuzi yakinifu imekamilika na Kazi ya
usanifu wa kina inayofanywa na Kampuni ya Crown
Tech-Consult ya
·
Upembuzi
Yakinifu, Usanifu wa Kina na kuandaa Nyaraka za Zabuni (Feasibility Study, Detailed Engineering Design and Preparation of
Tender Documents) kwa barabara ya
Mpanda-Koga-Tabora yenye urefu wa km.359 unaendelea vizuri kwani kazi ya
Upembuzi Yakinifu, Usanifu wa kina na kuandaa nyaraka za zabuni kwa ajili ya
ujenzi wa barabara ya Mpanda-Koga-Tabora kwa kiwango cha lami inayofanywa na
Kampuni ya COWI A/S kutoka Denmark na COWI Tanzania inaendelea.
·
Ukarabati
na Matengenezo ya Barabara Kuu na za Mkoa kupitia mpango wa PMMR (Performance Based Management and Maintenance
of Roads) km.363.78 kwa gharama ya Shilingi 8,438,063,163.02 unaendelea
vizuri. Tumeomba barabara zingine
ziingizwe katika mpango huu ili kufidia kilomita zilizoingizwa kwenye ujenzi wa
barabara ya Sumbawanga-Namanyere-Mpanda kwa kiwango cha lami. Aidha tumeziagiza Halmashauri zetu zijifunze
kuhusu utekelezaji wa PMMR ili
·
Wakati
mkoa unaanza hakukuwepo na simu za mkononi. Ilipofikia mwaka 2005, mtandao wa
simu za mkononi ulikuwa unapatikana Makao Makuu ya Wilaya tu. Leo, 2011, simu
za mkononi zinapatikana karibu Mkoa mzima wa Rukwa hadi maeneo ya mipakani mwa
Chunya (Mbeya), Mishamo karibu na Kigoma na mpakani mwa
·
Kiwanja
cha Ndege cha Mpanda kimeboreshwa na sasa kinajengwa kwa kiwango cha lami.
3.7 WATUMISHI.
Kwa muda wa miaka 50 ya Uhuru mkoa umekuwa na
upungufu wa watumishi katika sekta zote.
·
Kuanzisha na kusajili “Mfuko wa Kuboresha Mazingira ya Watumishi” mwaka 2006 ili kuvutia watumishi wanaopangwa kufanya kazi mkoani Rukwa, kwa
kutoa vivutio kwa watumishi wanaokubali kuja kufanya kazi Rukwa. Halmashauri
zote zinachangia mfuko huu kila mwaka, ambao umesaidia
·
Mkoa umeendelea kupanua na kuboresha elimu ya
Sekondari ili kupata vijana wengi wa Mkoa huu ambao tunaamini haitakuwa kikwazo
kwao kufanya kazi Rukwa.
·
Mkoa umeendelea kutoa mafunzo ya muda mfupi na muda
mrefu kwa watumishi ili kuwaendeleza watumishi waliopo.
·
Mwaka 1961 walikuwepo watumishi wachache waliokuwa
wamesoma na wasiokuwa na ujuzi wa kutosha, suala la kuwaendeleza watumishi
limeanza miaka ya 2007 hadi mwaka 2011 ambapo Sekretarieti ya Mkoa imepeleka
masomoni watumishi 78 kuanzia ngazi ya cheti hadi shahada ya pili.
3.8 HALI YA
UWEKEZAJI MKOA WA RUKWA.
Hali
ya Uwekezaji katika Mkoa wa Rukwa kuanzia mwaka 1961 hadi mwaka 2000 haikuwa
nzuri, lakini kuanzia mwaka 2000 hadi 2011 Mkoa unafanya vizuri katika
uwekezaji, kwa kuzinadi fursa mbalimbali zilizopo, baada ya Warsha ya Uwekezaji
ya Juni 2007 Wawekezaji walioitikia
wito wa kuwekeza Mkoani Rukwa ni:-
1. Mikebuka Fisheries Ltd. - Kununua na kusafirisha
samaki.
2. Energy Milling Ltd. -Usindikaji nafaka hususani mahindi na
mpunga.
3. Malonje Heritage Farm -
Ufugaji ng’ombe wa maziwa na usindikaji bidhaa za maziwa.
4. Brand International Ltd - Uchimbaji wa Madini ya
risasi- Mpanda.
5.Barka Milling
-Kusindika nafaka Malangali–Sumbawanga(ujenzi unaendelea).
6.
Executive Lodges - Hoteli – Sumbawanga.
7.
Katavi Hippopotamus - Hoteli Sitalike – Mpanda.
8.
Katavi Tented Hotels - Camp site Katavi – Mpanda.
9. Blue Water Tanzania LTD -Kiwanda cha Maji Sumbawanga (ujenzi
unaendelea).
10. Lake shore Lodge & Campsite - Hoteli ya kitalii
Kipili Nkasi.
11. SAAFI MEAT Ltd. Co
- Kiwanda cha kusindika nyama kilichopo Mjini Sumbawanga.
Wawekezaji Wengine.
Wawekezaji
walioonesha nia na waliofika kutembelea Mkoa wetu ni Kampuni ya ‘NO TILL’
kutoka Australia, Vetex Consultants (USA), Kiwanda cha Bia (TBL) na Agrisol (T)
Ltd wanaotaka kuwekeza kwenye kilimo na usindikaji wa mazao ya kilimo. Wengine
ni Tanzania Strategic Development Ltd kwa kushirikiana na Kampuni ya Upendo
wanataka kuzalisha nishati ya umeme kwa kutumia makaa ya mawe na Indian Mining
Co. wanaotaka kuwekeza kwenye uchimbaji Madini.
CHANGAMOTO KUU
ZINAZOKABILI MKOA.
·
Mkoa una upungufu mkubwa
wa watumishi katika sekta zote na wengi wao ni wale wenye ujuzi usiokidhi. Pia
kutokana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi shule nyingi za sekondari na
msingi zimejengwa. Kwa hali hii kuna upungufu mkubwa wa walimu, vifaa na samani.
·
Mkoa bado unakabiliwa na
tatizo kubwa la upatikanaji wa umeme wa uhakika kwani kwa sasa makao makuu ya
mkoa yanapata umeme kutoka nchi ya jirani ya Zambia, Namanyere na Mpanda
zinatumia Jenereta.
·
Kuwepo kwa miundombinu
mibovu hususan barabara katika maeneo mengi ya mkoa wa Rukwa na mawasiliano ya
msimu ya anga kupitia viwanja vidogo vya ndege vya Sumbawanga na Mpanda.
·
Kutokuwepo kwa wawekezaji wa maendeleo kwa
muda mrefu katika Mkoa wa Rukwa na hivyo kusababisha Maliasili kama ardí,
madini na wanyama pori kutowanufaisha wananchi.
·
Mkoa unakabiliwa na
kuwepo kwa gharama kubwa za matengenezo ya barabara, kutokana na kutokuwepo kwa
Kituo cha Ukodishaji wa Mitambo ya Ujenzi katika Mkoa wa Rukwa (kama ilivyo
Mbeya).
7. MIPANGO YA
KUKABILIANA NA CHANGAMOTO.
·
Mkoa utaendelea kupanua
na kuboresha elimu ya ngazi zote ili kupata vijana wengi wa mkoa huu ambao
tunaamini haitakuwa kikwazo kwao kufanyakazi Rukwa.
·
Kuimarisha mfuko wa
kuboresha mazingira ya watumishi ili uweze kutoa huduma kwa sekta zote kwa
kuwavutia watumishi wengi zaidi.
·
Kuendelea kushawishi
serikali na wawekezaji wengine kuwekeza katika upatikanaji wa umeme wa uhakika
mkoani.
·
Mipango iliyopo ni
kutengenezwa kwa kiwango cha lami barabara kuu tatu za Tunduma – Sumbawanga,
Sumbawanga- Kasanga na Sumbawanga – Namanyere - Kibaoni - Mpanda. Pia viwanja
vidogo vya ndege vya Sumbawanga na Mpanda vinakarabatiwa ili viweze kutoa
huduma ya usafiri wa anga kwa mwaka mzima.
·
Mkoa unaendelea
kushawishi wawekezaji kuja kuwekeza na wanaendelea kujitokeza.
·
Kuna mchakato wa ujenzi
wa Chuo Kikuu cha Kilimo Wilayani Mpanda ili kuweza kuongeza wigo wa wataalam
wa kilimo na kutoa nafasi ya ajira kwa wakazi wa mkoa wa Rukwa na Tanzania kwa
ujumla.