|
|
BEST STUDENTS IN RUKWA REGION REWARDED Mkuu wa mkoa wa Rukwa atimiza ahadi ya kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mtihani wa kidato cha nne mkoa wa Rukwa. Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Daniel Ole Njolay ametimiza ahadi yake aliyoiweka ya kula chakula cha pamoja na wanafunzi kumi bora waliofaulu vizuri katika mtihani wa kidato cha nne 2010/2011 katika mkoa wa Rukwa ikiwa ni pamoja na kuwapa zawadi ya shiilingi alfu hamsini kila mmoja. Mkuu wa mkoa alitoa ahadi hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibuni. Hafla hiyo ilifanyika siku ya ijumaa tarehe 18/02/2011 katika club ya country mjini Sumbawanga na kuhudhuriwa na maafisa elimu wa wilaya zote tatu (Sumbawanga, Nkasi na Mpanda),viongozi wa shule na wakuu wa wilaya ya Sumbawanga, Nkasi na Mpanda. Hiyo ilikuwa ni hatua mojawapo ya Mkuu wa Mkoa katika kutoa motisha kwa wanafunzi hao na wengine waweze kufanya vizuri zaidi ikiwa ni hatua za serikali ya mkoa kuboresha elimu. Katika kumi bora, wote walikuwa wanaume. Kutokana na kutokuwepo na mwanamke katika hao mkuu wa mkoa aliagiza kwa wale wasichana waliopata daraja la kwanza wajumuike nae katika hafla hiyo, hiyo ilikuwa ni katika kuleta usawa na kuwapa motisha wanawake ili nao waweze kufanya vizuri katika mitihani yao. Hata hivyo wanafunzi wote walioalikwa hawakuweza kuhudhuria katika hafla hiyo kutokana na baadhi yao kuwa safarini nje na mkoa wa Rukwa. Hakikuharibika kitu kwani waliwakilishwa na waalimu wao. Wanafunzi hao walimshukuru mkuu wa mkoa kwa kuwaalika kula nae na kuwapa zawadi, na kusema kwao hiyo ni kama changamoto ya kuweza kufanya vizuri zaidi katika masomo yao huko waendako.
|
|
||||||||||||||||||||