WARSHA YA PROGRAMU YA KUENDELEZA BIASHARA
SIDO mkoa wa Rukwa iliandaa warsha ya siku moja yenye lengo la kuwaendeleza wajasiriamali. Warsha hii iliendeshwa katika ofisi za SIDO mjini Sumbawanga na kuhudhuriwa na wajasiriamali 37. Mpango ambao ulianzishwa na mfuko wa sekta binafsi Tanzania katika programu ya BDG (Fanikiwa kibiashara)
Hii ni warsha ya awali baada ya wajasiriamali kujaza fomu na kueleza matatizo ya biashara ambazo zilichambuliwa na wataalamu toka SIDO na kupelekea kuandaa warsha hii ili kutoa ushauri wa kitaalamu ambao umelenga kuwasaidia wajasiriamali kuandaa mipango kazi na kuendeleza biashara zao. Mipango kazi mbalimbali itakayoandaliwa na wajasiriamali hao itachambuliwa na SIDO kabla ya kuiwasilisha BDG kwa ajili ya kushindanishwa na nyinginezo toka mikoa mingine, wale watakaofanikiwa kuwa na mipango kazi bora watazawadiwa dola 1,000 na Mfuko wa sekta binafsi Tanzania . Baada ya hatua hii ya awali mafunzo haya yataendelezwa kwa hatua nne tofauti na kila atakayefanikiwa kuvuka kila hatua atakua anazawadiwa dola 1,000 kwa hiyo atakayefanikiwa kuvuka hatua zote nne atapata dola 4,000. |