JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
MALIASILI NA MAZINGIRA
 
[ Natural Resources ] Environmental [ Home ] or
 

MAZINGIRA

 
 
 
 
Utangulizi
 

Mkoa una eneo lenye Km 2 75,250 kati ya hizi 68,645 km 2 ni nchi kavu na 6,605 km 2 ni eneo la maji. Shughuli mbambali za kibinadamu zinazoendelea katika Mkoa ambazo ni uvuvi, kilimo, ufugaji, uchimbaji madini na viwanda.

Zaidi ya wakazi 80% wanategemea kilimo kama uti wa mgongo wa Mkoa, mazao yanayolimwa ni pamoja na alizeti, mahindi, mpunga, maharage, ulezi, karanga na tumbaku. Tumbaku hulimwa zaidi maeneo ya Wilaya ya Mpanda.

 
 
 

Mkoa una mapori makubwa yaliyozungukwa na misitu na hifadhi za wanyama. Maeneo yenye misitu ni Ha. 2,826,288.3 na mapori ya Hifadhui za wanyama ni Km 2 21,703

Mkoa una ziwa Tanganyika na ziwa Rukwa, pamoja na haya maziwa mawili yapo maziwa mengine madogo ambayo ni ziwa Sundu, ziwa Katavi, Ziwa Chada, ziwa Kwela. Samaki wanaopatikana katika maeneo haya ni pamoja na:-

 

•  Mikebuka – lates stappersii

•  Sangara – lates mariae

•  Dagaa – limnothrissa miodon

– stolothrissa tanganicae

•  Singa –dinotropterus cunnington

•  Kuhe – Boulengerochromis michrolepsi

•  Samaki – Acquarious spp (ornamental fish)

Kutokana na ongezeko la watu kwa asilimia 3.6 kwa mwaka kutokana na sensa ya mwaka 2002, hivyo kufanya maeneo mengi kuvamiwa kwa ajili ya shughuli za kibinadamu, ambapo inakdiriwa zaidi ya Ha. 85,000 zimeharibiwa kutokana na uvamizi huo

 
 

CHANGAMOTO

Muamko mdogo wa wananchi dhidi ya hifadhi ya mazingira kumepelekea kutoweka kwa uoto wa asili kwani wakazi wake asilimia 80 hutegemea nishati ya kuni kama njia pekee ya nishati.

Pamoja na hali hiyo yapo mashirika ya umma yanayojishughulisha na uhifadhi wa mazingira Mkoani Rukwa ambayo ni KAESO, REYO, TATEDO WSC, haya yote yanahamasisha wananchi kuhifadhi mazingira kwa njia mbalimbali zikiwemo matumizi ya majiko banifu,uboreshaji wa mazingira kwa njia ya upandaji miti.

Kupitia mpango wa kuweka miji safi programu ya UDEM imehakikisha kuwa mazingira ya miji yanakuwa safi kwa kuanzisha vikundi kazi vitavyoshughulikia kero mbalimbali,

 
 
 
         
 
[ Natural Resources ] Environment [ Home ] or
Go up
 
     
Copyright © 2008 -Rukwa Regional Commissioner's Office,SUMBAWANGA, TEL: 025- 2802137/2802138, FAX: 025-280-2217/2144/1001