• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Manispaa ya Sumbawanga yatoa 115% ya fedha za uwezeshaji kiuchumi

imewekwa Tar: June 29th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameisifu Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa kuzidisha kiwango cha asilimia 10 ya mikopo kwa Vijana, akina Mama na Watu wenye Ulemavu kwa kutoa shilingi 253,228,000/= zaidi ya lengo la awali ambapo halmashauri ilitakiwa kutoa Shilingi 2,212,104,000/= kutokana na makisio ya makusanyo yake ya ndani yaliyolenga kukusanya Shilingi 2,212,104,000/=.

Mh. Wangabo alisema kuwa kiwango hicho cha asilimia 10 ambachoo Manispaa ya Sumbawanga wameweza kukitoa ni sawa na asilimia 115 kutokana na mapato yaliyokusanywa ya shilingi Bilioni 3.1 ambayo ni tofauti na makadirio yaliyofanyika kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

“Taarifa ya Mkurugenzi imeonesha kuwa kuna mafanikio ya kujivunia katika suala zima la uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kipindi cha Miaka sita, kiwango cha fedha kinachotolewa kama mtaji kwa wajasiriamali kimekuwa kikiongezeka kila Mwaka na kwa Mwaka huu wa fedha 2018/2019 Manispaa imevunja rekodi kwa kutoa Shilingi 253, 228,000/= jambo hili ni la kupongezwa kwa mafanikio mliyofikia ya kutoa fedha 10% ya mapato ya ndani kwa 115% haya ni mafanikio makubwa sana, hivyo Hongereni sana Manispaa ya Sumbawanga,” Alisema.

Aidha, aliupongeza uongozi mzima wa Wilaya ya Sumbawanga pamoja na Halmashauri hiyo kwa kutekeleza sheria ya fedha ya mwaka 2018 inayoelekeza utekelezaji wa uwezeshaji wa vijana, kinamama na watu wenye ulemavu na kuzitaka halmashauri nyingine za mkoa kuiga mfano huo na hatimae kuwafaidisha wananchi kwa mikopo isiyo na riba ili waweze kujiinua kiuchumi.

Wakati akisoma taarifa ya utoaji wa mikopo Mkurugenzi wa manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya alisema kuwa siku ya leo (28.6.2019) Halmashauri itatoa mikopo kwa vikundi 32 ambapo kati ya hivyo vikundi vya Wanawake 13, Vijana 14 na Watu wenye Ulemavu 5 ambapo kiasi cha Tsh. 73,678,000 kitatolewa kama uwezeshaji wa Wananchi.

“Kwa maana hiyo, Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa kipindi cha mwaka 2018/19 itakuwa imeweza kutoa mikopo kwa vikundi 114 vikiwemo vya Wanawake 56, Vijana 44 na watu wenye ulemavu 14 Ambapo kiasi cha jumla ya Tshs. 253,228,000.00 zitakuwa zimetolewa kwa makundi yaliyoainishwa. Hivyo itapelekea kufikiwa kwa jumla ya wanachama 1,135 kama wanufaika wa mikopo hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019,” Alieleza.

Pamoja na mafanikio hayo makubwa, Mtalitinya hakusita kugusia changamoto ambazo halmashauri inakumbana nazo ikiwemo Hamasa ndogo ya uanzishwaji wa vikundi vya kiuchumi, Uelewa mdogo wa Jamii kuhusu uanzishwaji wa vikundi vya kiuchumi, Uelewa mdogo wa fursa za kiuchumi kwa Jamii. Kukosekana kwa masoko ya bidhaa za vikundi. Na hivyo kuahdi kuendela kutoa elimu  ya ujasiriamali kwa vikundi  ngazi ya kata na mitaa.

Katika hatua nyingine Mh. Wangabo alichukua fursa hiyo kukabidi kikombe cha ushindi wa jumla wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2018 ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga iliibuka na ushindi huo.  

Matangazo

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2019 - Rukwa October 17, 2019
  • Waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza Mkoa wa Rukwa 2018 January 05, 2018
  • Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) October 09, 2018
  • Kikao cha Road Board Mkoani Rukwa October 08, 2018
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Utoro, Uvivu na kutoshirikisha wazazi kwatajwa kuwa kikwazo cha ufaulu Rukwa.

    December 06, 2019
  • Mawakala wa Mbolea watolewa wasiwasi huku wakulima wakikataa rangi ya mbolea Inbox x

    December 03, 2019
  • Wanarukwa wahamasishwa kulima kwa tija ili kujiongezea kipato

    December 02, 2019
  • TARURA watakiwa kushughulikia maeneo korofi msimu wa mvua

    November 30, 2019
  • Angalia Zote

Video

Kisa Kamili cha Mama Mjamzito Kujijeruhi tumboni chafafanuliwa na RMO Rukwa
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Kilio cha Wananchi kinasikilizwa
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Regional Block, 90 Mwl. Julius Nyerere Road

    Sanduku la barua: Box 128 Sumbawanga

    Simu: 025 280 2137

    Simu: 0756941328

    barua pepe: ras@rukwa.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa