• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

RC Rukwa asisitiza mambo matatu kwa madiwani kikao cha PS3

imewekwa Tar: May 16th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kmaishna Mstaafu Zelote Stephen amewasisitiza madiwani kufuatilia miradi, kusimamia mapato na utawala bora ili Halmashauri za mkoa wa Rukwa ziweze kuendelea na kufikisha huduma bora kwa wananchi.

Aliyasisitiza hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi pamoja na Manispaa ya Sumbawanga zote za Mkoa wa Rukwa siku ya tarehe 15 Mei, 2017. Mafunzo yanayoendeshwa na mradi wa PS3  unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la watu wa Marekani USAID.

Katika kuyafafanua kila jambo Mh. Zelote alianza kwa kuwasisitiza waheshimiwa Madiwani Kufuatilia na kufanya tathmini ya miradi yote inayotekelezwa na Halmashauri zetu.

Mh. Zelote aliwakumbusha fedha zinazotoka Serikali kuu na kupelekwa Serikali za Mitaa na kutumika katika utekelezaji wa miradi ya sekta mbalimbali ikiwemo, Elimu, Afya, Maji, Barabara namengineyo. Hivyo aliwasisitiza kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa ubora unaotarajiwa.

“Nimekuwa nikifanya ziara nyingi sana katika kata mbalimbali zenye miradi hii, na nikifika huko naona namna miradi hiyo inavyotekelezwa chini ya viwango mpaka huwa najiuliza hivi kuna diwani kweli kwenye kata hii, mbona miradi hii ambayo ni faida kwa wananchi inakuwa haieleweki?” Mh. Zelote alieleza.

Kwa upande wa kusimamia mapato Mh. Zelote aliwatahadharisha madiwani hao kuwa kama Halmashauri haitakusanya mapato ya kutosha maana yake Halmashauri haitakuwepo jambo litakalopelekea wananchi kukosa huduma muhimu na kucheleweshewa maendeleo.

“Watumishi wote katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wafanye kazi kwa juhudi na maarifa na pia waepuke kufanya kazi kwa mazoea ili kuimarisha ukusanyaji wa mapato, na Wakurugenzi wa halmashauri zote wasimamie vizuri ukusanyaji wa mapato,” Mh. Zelote alisisitiza.

Katika kuhakikisha madiwani wanaelewa maana ya utawala bora katika kupeleka maendeleo kwa wananchi Mh. Zelote alisisitiza kuwa maendeleo hayana vyama, dini, ukabila na kwamba wadau wote wa maendelo wanapaswa kushirikiana kwa pamoja ili wananchi wote wapate maendeleo kwa usawa.

Mkuu wa Mkoa alisema, “Ili wananchi wawe ni sehemu ya maendeleo ya miradi inayopelekwa katika maeneo yao basi waheshimiwa madiwani ndio madaraja ya kupeleka maendeleo hayo, hivyo wao wanatakiwa kuwa kitu kimoja na kuachana na itikadi za kisiasa ili kuwafikishia wananchi maendeleo.”

Katika kukazia yale aliyoyazungumza Mh. Zelote aliwaomba madiwani hao kuyatumia vizuri mafunzo hayo yaliyotolewa na mradi wa Public Sector Strengthening System (PS3) na kuwashukuru watu wa Marekani ambao kwa kupitia shirika lao la Maendeleo USAID wameweza kufadhili mafunzo hayo.

Matangazo

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2019 - Rukwa October 17, 2019
  • Waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza Mkoa wa Rukwa 2018 January 05, 2018
  • Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) October 09, 2018
  • Kikao cha Road Board Mkoani Rukwa October 08, 2018
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Utoro, Uvivu na kutoshirikisha wazazi kwatajwa kuwa kikwazo cha ufaulu Rukwa.

    December 06, 2019
  • Mawakala wa Mbolea watolewa wasiwasi huku wakulima wakikataa rangi ya mbolea Inbox x

    December 03, 2019
  • Wanarukwa wahamasishwa kulima kwa tija ili kujiongezea kipato

    December 02, 2019
  • TARURA watakiwa kushughulikia maeneo korofi msimu wa mvua

    November 30, 2019
  • Angalia Zote

Video

Kisa Kamili cha Mama Mjamzito Kujijeruhi tumboni chafafanuliwa na RMO Rukwa
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Kilio cha Wananchi kinasikilizwa
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Regional Block, 90 Mwl. Julius Nyerere Road

    Sanduku la barua: Box 128 Sumbawanga

    Simu: 025 280 2137

    Simu: 0756941328

    barua pepe: ras@rukwa.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa