• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Waaswa Watumishi Wa Serikali Mipakani Kutoisaliti Nchi Yao Kujiepusha Na Ugonjwa Wa Corona

imewekwa Tar: March 28th, 2020

Katika hali ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona, Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka maafisa uhamiaji pamoja na watumishi wengine katika bandari za mkoa huo pamoja na mpaka wa nchi kavu kuacha tabia ya kupokea rushwa kutoka kwa wageni hasa katika kipindi hiki ambacho ni hatari kwa nchi.

Mh. Wangabo amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa kwani kuwapitisha wageni hao kwa kutumia rushwa kutasababisha nchi itaingia kwenye madhara makubwa ikiwemo kuliangamiza taifa na kuongeza kuwa kufanya hivyo ni sawa na usaliti kwa nchi, hivyo aliwataka watumishi hao kuwa wazalendo na nchi yao, kwani kutofanya hivyo kuna uwezekano wa kupitisha mgonjwa mmoja ambae ataweza kupelekea madhara makubwa katika nchi.

“Kwahiyo muwe makini sana, vitendo vya rushwa marufuku na kila jambo lichukuliwe kwa umuhimu na uzito mkubwa sana, kumbukeni kwamba kwenye mipaka ndipo mmebeba taifa, kwasababu atakayepitishwa pale bila ya kuzingatia taratibu zinazotakiwa, bila ya kuchunguzwa vizuri, bila ya kuulizwa ulizwa vizuri historia alikotokea na kumuweka katika “isolation room” kama itabidi kulingana na atakavyokuwa ameonekana, msipofanya hivyo mtu akapita, basi mjue kabisa kwamba analeta vifo katika nchi yet una huo utakuwa ni usaliti kwasababu umelisaliti taifa kwa kupitisha mtu ili aje atuue,” alisisitiza.

Mh. Wangabo ameyasema hayo alipotembelea katika bandari ya Kabwe iliyopo katika kata ya Kabwe, Wilayani Nkasi ili kukagua utekelezaji wa maelekezo ya serikali juu ya kuandaa maeneo maalumu kwaajili ya kuwaweka wageni kwa siku 14 pamoja na kuona kituo cha huduma ya afya kilichotengwa maalum kwaajili ya kuwapokea watu wanaodhaniwa kuwa na ugonjwa wa Corona kwa uangalizi zaidi ambapo katika ziara hiyo aliambatana na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa pamoja na wataalamu wengine.

Aidha, Mh. Wangabo ameutaka uongozi wa Wilaya kuhakikisha wanatoa elimu ya udhibiti wa ugonjwa wa Corona kwa wenyeviti wa vijiji vyote vilivyopo katika mwambao wa ziwa Tanganyika kwani imebainika kuwa mara kadhaa vijiji hivyo hutumika kama bandari zisizo rasmi kuingiza wageni wanaotoka katika nchi za Jamhuri ya Watu wa Kongo, Burundi pamoja na Zambia.

Wakati akitoa taarifa ya maandalizi ya kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo wa Corona Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Dkt. Hashim Mvogogo amesema kuwa majengo ya Hospitali ya Wilaya yamepangwa kutumika kuhifadhi wagonjwa watakaobainika kuwa na Virusi vya Corona baada ya siku 14 na pia kutumika kama kituo cha tiba endapo wagonjwa hao watatokea na kuongezeka na kuongeza kuwa kata 21 na vijiji 62 vimeshapewa elimu ya afaya ya kujikinga na ugonjwa huo huku wananchi wakionekana kuelewa na kuhamasika.

“Katika Kata tumetumia wasimamizi wa afya, ndio maana ukiangalia hata katika baadhi ya shule kabla hazijafungwa tulizifikia shule 42, kwahiyo tulianza “intervention” mapema kwa maana ile timu ya Wilaya hatukuweza kufika kwenye hizo sehemu lakini tulitumia wataalamu wetu ambao wako katika zile sehemu, kwahiyo kiujumla kama elimu kiwilaya wote, karibia kata zote wanahiyo elimu, lakini zile kata ambazo hatukufikia wataalamu kutoka ngazi ya wilaya, tunahitaji pia tuzifikie na sisi,” Alisema.

Kwa upande wake Mwangalizi wa Bandari ya Kabwe Mohamed Issa amesema kuwa mbali na kutenga nyumba mojawapo ya mtumishi kwaajili ya kuwahifadhi wageni watakaoingia nchini kwa siku 14, pia kuna boti maalum ambayo imeandaliwa kwaajili ya kufanya doria katika badari bubu zaidi ya nne zilizopo katika vya karibu na bandari hiyo ili kujihadhari na uingiaji holela wa wageni hao.

“Boti hii ni kwaajili ya kufanya “patrol” kwenye bandari bubu ambazo ni pamoja na Utinta, Kalila, Korongwe na Msalamba ndio bandari bubu ambazo zinatumiwa na wafanyabiashara ambao sio waaminifu wanaokwepa mapato ya serikali, kwahiyo hii boti itatusaidia kufika maeneo hayo kwa urahisi ili pia kulinda mapato ya serikali,” Alisema. Katika Wilaya ya Nkasi kuna bandari bubu zaidi ya 12 ambazo hutumika na wageni kuingia nchini huku bandari rasmi zinaz otambulika ni 3 ikiwemo, Kirando, Kabwe na Wampembe ambapo bandari hiyo ya ipo katika hatua za mwisho kumalizika kutanuliwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 7.4 na ujenzi wake kufikia asilimia 95% hali iliyopelekea Mh. Wangabo kuwataka wananchi wa Mkoa wa Rukwa kuitumia bandari hiyo na fursa zake vizuri ili kujiingizia kipato.

Matangazo

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2019 - Rukwa October 17, 2019
  • Orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza Mwaka 2021, Mkoa wa Rukwa December 18, 2020
  • Fomu za Kujiunga na Shule mbalimbali za Sekondari (JOINING INSTRUCTION) kwa Mwaka 2021 mkoani Rukwa. December 20, 2020
  • Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) October 09, 2018
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Wananchi watakiwa kuacha kulalamika na badala yake waisaidie serikali ili kuijenga nchi.

    March 07, 2021
  • RC Wangabo atoa elimu ya kujikinga na majanga huku nyumba Zaidi ya 80 zikiezuliwa na upepo

    March 06, 2021
  • Mpango wa Mji wa Sumbawanga Kupata maji kutoka Ziwa Tanganyika unakaribia.

    March 02, 2021
  • RC Wangabo atoa neno baada ya DED kukataa kuhojiwa na madiwani na kumhusisha Rais Magufuli.

    March 01, 2021
  • Angalia Zote

Video

Mwaka 2020 kuwa mwaka wa kuwalinda watoto dhidi ya Ukatili Mkoani Rukwa
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Kilio cha Wananchi kinasikilizwa
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Regional Block, 90 Mwl. Julius Nyerere Road

    Sanduku la barua: Box 128 Sumbawanga

    Simu: 025 280 2137

    Simu: 0756941328

    barua pepe: ras@rukwa.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa