Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi
Shughuli za Uvuvi katika Mkoa, zinaathiriwa na vitendo vya Uvuvi haramu, uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi. Katika kukabiliana na changomoto hizo Mkoa umeendelea kuratibu usimamizi endelevu wa raslimali za Uvuvi kwa kutoa mafunzo ya Uvuvi endelevu na kufanya doria kwa kushrikiana na vituo vinne (4) vya usimamizi wa raslimali za uvuvi vilivyoko chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Kwa mwaka 2018/2019 doria zilizofanyika zilifanikisha kukamata kokoro 36 monofilamenti 22 makila chini ya inchi tatu 71 vyandarua vya mbu 41 mitumbwi isiyo na usajili 40, ringnet 18 (<8mm) na watuhumiwa 94 walihukumiwa.
Kuendeleza Ufugaji wa samaki katika mabwawa
Mkoa umetambua mabwawa 326 yanayofanya kazi ya uzalishaji wa samaki katika Halmashauri zote 4 na kuyasajili kwenye rejista ya wafugaji wa samaki. Sambamba na hilo Elimu ya Ufugaji samaki na utengenezaji wa vyakula vya samaki imetolewa kwa wafugaji 37.
Mikakati ya kuendeleza sekta ya Uvuvi
Ili kukabiliana na Changamoto za sekta ya Uvuvi Mkoa unaendelea kushauri na kuhimiza Halmashauri kutekeleza mikakati ifuatayo:-
Kuajiri wataalamu wa Uvuvi, lengo ni kuwa na maafisa ugani kwa kila Kata yenye mwalo.
Kutekeleza agizo la Ofisi ya Rais -TAMISEMI la kutenga fedha 5% ya mapato yatokanayo na Uvuvi kwa ajili ya kuwezesha kudhibiti Uvuvi haramu katika Maeneo yao na kuendelea kutoa elimu ya uvuvi endelevu.
Kuwezesha mazingira bora ya uundwaji wa vikundi vya uvuvi endelevu (BMUs) na kuvisajili ili vifanye kazi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Uvuvi.
Kuendelea kuvutia wawekezaji ili wajenge viwanda vya kuchakata mazao ya uvuvi ili kuyaongezea thamani, wawekeze katika biashara ya samaki wa mapambo.
Kuendeleza ufugaji wa samaki katika Mabwawa na katika vizimba(cage culture) ili kuongeza mazao ya Uvuvi na kupunguza utegemezi mkubwa katika maziwa yetu.
Kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika maduka na zana halali, bora na za kisasa za uvuvi
Mwanamama Kutoka Kasanga Wilaya ya Kalambo akiwa ameshika Samaki wa Ziwa Tanganyika
Kasanga, Wilayani Kalambo, Ziwa Tanganyika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 1 Barabara ya Mkoani
Sanduku la barua: Box 128 Sumbawanga, 55180 RUKWA
Simu: 025 280 2137
Simu: 0739862632
barua pepe: ras@rukwa.go.tz
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa