Mkoa wa Rukwa ulianzishwa mwaka 1974 kwa kumega sehemu ya Mkoa wa Tabora (Mpanda) na Mbeya (Sumbawanga). Mnamo mwezi Julai 2010 Serikali ya Awamu ya Nne iliridhia kugawanywa kwa Mkoa wa Rukwa na kuanzishwa kwa Mkoa mpya wa Katavi.
Jiografia ya Mkoa
Mkoa wa Rukwa upo kati ya Latitudo 70 – 90 Kusini ya Ikweta na Longitudo 30 – 320 Mashariki ya Grinwichi. Mkoa huu unapakana na Mikoa ya Katavi upande wa Kaskazini na Songwe upande wa Kusini Mashariki; Aidha, unapakana na nchi za Zambia upande wa Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa Magharibi. Eneo la juu sana katika Mkoa wa Rukwa linapatikana Malonje katika Nyanda za juu za Ufipa ambalo ni Mita 2,461 Juu ya Usawa wa Bahari na eneo la chini zaidi ni Ziwa Tanganyika lenye Mita 773 Juu ya Usawa wa Bahari.
Eneo la Mkoa
Mkoa huu una eneo la kilomita za mraba 27,765, kati ya hizo Kilomita za mraba 22,844 (82.3%) ni za nchi kavu na Kilomita za mraba 4,921 (17.7%) ni za maji kama ilivyoainishwa katika Jedwali
Eneo Mkoa wa Rukwa mwaka 2017
Wilaya
|
Halmashauri ya Wilaya/ Manispaa
|
Eneo Km. za mraba
|
Eneo la Ardhi.
|
Eneo la Maji.
|
||
Km2
|
%
|
Km2
|
%
|
|||
S’wanga
|
S’wanga MC
|
1,329
|
1,329
|
100.0
|
0
|
0
|
S’wanga DC
|
8,871
|
8,203
|
92.5
|
668
|
7.5
|
|
Nkasi
|
Nkasi
|
13,124
|
9,375
|
71.4
|
3,749
|
28.6
|
Kalambo
|
Kalambo
|
4,441
|
3,937
|
88.7
|
504
|
11.3
|
Jumla
|
|
27,765
|
22,844
|
82.3
|
4,921
|
17.7
|
Muundo wa Mkoa Kiutawala
Mkoa wa Rukwa umegawanyika katika Wilaya tatu (3), zenye Halmashauri nne (4), Tarafa 16, Kata 97, Vijiji 339 Vitongoji 1,825 Kaya 185,076 na Mitaa 167. Wilaya hizo ni Sumbawanga, Kalambo na Nkasi. Mkoa unajumuisha Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Nkasi na Kalambo. Aidha, ndani ya Mkoa kuna Mamlaka za Miji Midogo miwili ambazo ni Namanyere Wilaya ya Nkasi na Laela Wilaya ya Sumbawanga. Yapo majimbo matano (5) ya Uchaguzi ambayo ni: Sumbawanga Mjini na Kwela – Wilaya ya Sumbawanga; Kalambo – Wilaya ya Kalambo; Nkasi Kusini na Nkasi Kaskazini – Wilaya ya Nkasi.
Eneo la Muundo wa Utawala Mkoa wa Rukwa 2017
Wilaya
|
Halmashauri
|
Eneo Km. Za mraba
|
IDADI YA
|
|||||
Tarafa
|
Kata
|
Vijiji
|
Vitongoji
|
Mitaa
|
Majimbo ya Uchaguzi
|
|||
S’wanga
|
S’wanga MC
|
1,329
|
2
|
19
|
24
|
173
|
167
|
1
|
S’wanga DC
|
8,871
|
4
|
27
|
114
|
494
|
0
|
1
|
|
Nkasi
|
Nkasi
|
13,124
|
5
|
28
|
90
|
721
|
0
|
2
|
Kalambo
|
Kalambo
|
4,441
|
5
|
23
|
111
|
439
|
0
|
1
|
Jumla
|
|
27,765
|
16
|
97
|
339
|
1825
|
167
|
5
|
Idadi ya Watu
Kwa mujibu wa Sensa ya watu na Makazi ya Mwaka 2012, Mkoa wa Rukwa ulikuwa na Wakazi wapatao 1,004,539 ambapo Wanawake ni 517,228 na Wanaume ni 487,311. Mkoa pia unazo Kaya 185,076 na wastani wa wakazi kwa Kaya moja ni watano (5). Ongezeko hili ni sawa na wastani wa asilimia 3.2% kwa Mwaka.
Mwaka 2017 Mkoa unakisiwa kuwa na Wakazi wapatao 1,192,373 ambapo Wanawake wanakisiwa kuwa 613,942 na Wanaume 578,431 Mchanganuo wa takwimu za idadi ya watu na makazi kwa mwaka 2012 na maoteo ya mwaka 2017 ni kama ilivyo katika jedwali
Idadi ya Wakazi Kiwilaya kwa Mwaka 2012
|
|||||
HALMASHAURI
|
IDADI
|
WAKAZI KWA KAYA
|
|||
ME
|
KE
|
JUMLA
|
KAYA
|
WASTANI
|
|
Sumbawanga MC
|
100,734 |
109,059 |
209,793 |
41,644 |
4.8 |
Sumbawanga DC
|
149,062 |
156,784 |
305,846 |
52,084 |
5.0 |
Nkasi DC
|
137,041 |
144,159 |
281,200 |
50,597 |
5.3 |
Kalambo DC
|
100,474 |
107,226 |
207,700 |
40,751 |
4.9 |
Jumla
|
487,311 |
517,228 |
1,004,539 |
185,076 |
5.0 |
Maoteo ya Idadi ya Wakazi Kiwilaya kwa Mwaka 2017
|
|||||
HALMASHAURI
|
IDADI
|
WAKAZI KWA KAYA
|
|||
ME
|
KE
|
JUMLA
|
KAYA
|
WASTANI |
|
Sumbawanga MC
|
119,570 |
129,451 |
249,021 |
51,879 |
4.8 |
Sumbawanga DC
|
176,934 |
186,100 |
363,035 |
72,607 |
5.0 |
Nkasi DC
|
162,666 |
171,115 |
333,780 |
62,977 |
5.3 |
Kalambo DC
|
119,261 |
127,276 |
246,537 |
50,313 |
4.9 |
Jumla
|
578,431 |
613,942 |
1,192,373 |
237,776 |
5.0 |
Hali ya hewa
Mkoa wa Rukwa una hali ya hewa ya Kitropiki ambapo wastani wa joto ni Sentigredi 13 katika baadhi ya maeneo kwa miezi ya Juni na Julai hadi Sentigredi 27 kwa miezi yenye joto jingi ya Oktoba na Desemba. Mkoa umebahatika kuwa na mvua za kuaminika kwa miaka mingi; mvua za Mkoa huu ni wastani wa milimita 850 kwa mwaka zikinyesha kuanzia mwezi wa Novemba – Mei. Kiangazi huanza mwezi Juni mara baada ya majira ya mvua hadi mwezi wa Oktoba.
Shughuli za Kiuchumi
Kiuchumi, wakazi wa Mkoa wa Rukwa wanajishughulisha na, Kilimo cha mazao ya chakula na biashara, ufugaji, sekta ya utalii, madini, uvuvi, viwanda vidogo pamoja na biashara ndogondogo. Shughuli kuu ya Kiuchumi ni Kilimo, ambapo mazao ya chakula yanayolimwa kwa wingi ni Mahindi, Mpunga, Viazi vitamu, Viazi mviringo, Mihogo, Maharage na Ulezi. Mazao ya biashara yanayolimwa kwa wingi ni Alizeti, Ngano, Ufuta na Michikichi. Aidha, ziada ya Mazao ya chakula kama Mahindi, Mpunga, Maharage, Ulezi, Ngano, Shayiri na Karanga hutumika pia kama mazao ya biashara. Ufugaji unabaki kuwa shughuli kuu muhimu ya pili ya uchumi katika Mkoa wa Rukwa. Mifugo inayofugwa kwa wingi ni Ng’ombe, Mbuzi, Nguruwe, Kondoo, Punda na Kuku.
Pato la Mkoa wa Rukwa
Pato la Mkoa limekuwa likiongezeka mwaka hadi mwaka, kutoka kiwango shilingi 2,718,398 (milioni) sawa na asilimia 3.41 mwaka 2014 hadi kufikia shilingi 3,180,865 (milioni) sawa na asilimia 3.50 mwaka 2015. Kuhusu pato la mwananchi kwa mwaka, nalo pia limekuwa likiongezeka kutoka shilingi 1,618,883 mwaka 2014, hadi kufika Shilingi 1,840,724 mwaka 2015. Hii ni kwa mujibu wa takwimu za mwisho zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mwaka huu 2016.
Historia ya Viongozi kwa Mkoa wa Rukwa
Orodha ya Wakuu wa Mkoa tangu mkoa ulipoanzishwa.
Na
|
Jina Kamili
|
Tarehe aliyoanza
|
Tarehe Aliyoondoka
|
1.
|
Mr. M.G. Baruti
|
1, Januari 1974
|
21, Februari 1983
|
2.
|
Mr. E.S. Mnyawami
|
22, Februari 1983
|
5, Juni 1984
|
3.
|
Mej. Gen. T. Kiwelu
|
6, Juni 1984
|
14, Novemba 1988
|
4.
|
Capt. P.N. Kafanabo
|
15, Novemba 1988
|
9, Disemba 1990
|
5.
|
Dr. K.M. Kiwanuka
|
10, Disemba 1990
|
8, Septemba 1991
|
6.
|
Mr. A.S. Aljabri
|
9, Septemba 1991
|
5, Novemba 1993
|
7.
|
Mr. C.M. Mzindakaya
|
6, Novemba 19993
|
30, Disemba 1995
|
8.
|
Mej. S. Nswima
|
31, Disemba 1995
|
10, Disemba 1997
|
9.
|
Capt. Jaka M. Mwambi
|
11, Disemba 1997
|
7, Februari 2003
|
10.
|
Capt. G.H. Mkuchika
|
8, Februari 2003
|
20, Agosti 2005
|
11.
|
Daniel Ole Njoolay
|
6, Februari 2006
|
15, Septemba 2011
|
12.
|
Eng. Stella Martin Manyanya
|
16, Septemba 2011
|
30, Agosti 2015
|
13.
|
Magalula Said Magalula
|
31, Agosti 2015
|
13, Machi 2016
|
14.
|
Zelote Stephen Zelote
|
13, Machi 2016
|
26, Oktoba 2017
|
15.
|
Joachim leonard Wangabo
|
26, Oktoba 2017
|
|
Orodha ya Makatibu Tawala wa Mkoa tangu kuanzishwa kwa Mkoa
Namba
|
Jina
|
Tangu
|
Mpaka
|
1.
|
J. Matiko
|
1.1.1974
|
29.3.1975
|
2.
|
D.F.P Ringo
|
30.3.1975
|
18.8.1976
|
3.
|
R.S. Lukindo
|
19.8.1976
|
6.1.1980
|
4.
|
S.K. Masinde
|
7.1.1980
|
2.1.1984
|
5.
|
C.T. Kisanji
|
2.1.1984
|
17.11.1985
|
6.
|
T.N. Machume
|
18.11.1985
|
16.2.1989
|
7.
|
A.A.K. Mwasajone
|
17.2.1989
|
17.2.1994
|
8.
|
P.A. M Chikira
|
20.5.1995
|
14.2.1997
|
9.
|
W. Ngirwa
|
15.2.1997
|
15.11.1998
|
10.
|
H.N.M. Kachechele
|
16.11.1998
|
3.4.2006
|
11.
|
Innocent Mwenda
|
4.4.2006
|
7.7.2009
|
12.
|
Salum .M.Chima
|
25.1.2010
|
18.1.2014
|
13.
|
Smythies E. Pangisa
|
18.1.2014
|
29.2.2016
|
14.
|
Tixon Tuyangine Nzunda
|
9.9.2016
|
23.5.2017
|
15.
|
Bernard Mtandi Makali
|
23.5.2017
|
|
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 1 Barabara ya Mkoani
Sanduku la barua: Box 128 Sumbawanga, 55180 RUKWA
Simu: 025 280 2137
Simu: 0739862632
barua pepe: ras@rukwa.go.tz
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa