Hiki ni kibali maalum cha Serikali kinachotolewa kwa mfanyabiashara yeyote anapotaka kufanya biashara hapa nchini. Sheria ya Leseni za Biashara Na. 25 ya 1972 – Kifungu cha 3(a) kimeweka bayana kuwa, Kibali hicho maalumu kinaitwa Leseni ya Biashara. Kwa hiyo basi, kufanya biashara yoyote bila kuwa na kibali hiki ni kosa la jinai.
Ili Mwombaji Apate Leseni Ya Biashara Anapaswa Kumbatanisha Nyaraka Zifuatazo:
1. Nakala ya hati ya kuandikisha jina la Biashara au Kampuni (Photocopy of Certificate of Incorporation or Registration & Extract
2. Nakala ya ushahidi wa maandishi kuwa ana mahali pa kufanyia biashara (lease agreement, Title deed, Certificate of occupancy, e.t.c);
3. Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi (Tax Payer Identification Number - TIN).
4. Hati ya uthibitisho wa ulipaji kodi (Tax Clearance Certificates
Mamlaka za Serikali za Mitaa(Halmashauri) zinahusika na utoaji wa Leseni za Biashara ambazo zinatambulika kama Leseni za Biashara za kundi B(Makundi yameainishwa katikaSheria ya Fedha na. 2 ya mwaka 2014). Ili kupata Leseni inatakiwa ufike Halmashauri ambayo unataka kufanyia biashara yako na kuwasilisha maombi yako pamoja na kupata maelekezo mengine ya taratibu za usajili wa Leseni ya Biashara.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 1 Barabara ya Mkoani
Sanduku la barua: Box 128 Sumbawanga, 55180 RUKWA
Simu: 025 280 2137
Simu: 0735019734
barua pepe: ras@rukwa.go.tz
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa