SEKTA YA MADINI
Umuhimu na nafasi ya sekta ya madini katika Mkoa.
Kama ilivyoelekezwa katika ibara ya 35 ya ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015- 2020 kuwa serikali ya Mkoa itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wanaohitaji kuwekeza katika madini.
Mkoa umesheheni rasilimali ya madini mbalimbali na vito. Hata hivyo, uchimbaji wa madini haya ni kwa kiasi kidogo na unaofanywa na wachimbaji wadogo. Mkoa unatambua umuhimu na nafasi ya madini katika kuchangia pato la taifa na la mwananchi mmoja mmoja. Kwa kulifahamu hilo, Mkoa unaweka mazingia mazuri ya upatikanaji wau meme, uboreshaji wa miundombinu ya barabara na mawasiliano ili kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza katika uchimbaji wa madini na vito ndani ya Mkoa.
Fursa za uwepo wa madini na vito zimetangazwa kwenye makongamano mbalimbali yaliyofanyika katika ndani na nje ya Mkoa (mwaka 2007 na Kanda ya Magharibi ya mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma miaka ya 2012, 2013 na 2014.) Aidha, maelezo hayo yanapatikana kwenye tuvuti ya Mkoa na Halmashauri.
Ofisi ya Madini Mkoa
Katika mwaka wa fedha 2018/19, Tume ya Madini ilifungua Ofisi ya Madini Mkoa wa Rukwa (RMO – Rukwa). Ofisi hii imeanza kazi tarehe 09/11/2018 na inasimamia shughuli zote za madini katika Wilaya zote za Mkoa wa Rukwa na Halmashauri zake (Nkasi, Kalambo, Sumbawanga Manispaa na Sumbawanga Vijijini).
Soko la Madini
Ofisi ya Madini Mkoa wa Rukwa kwa kushirikiana Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa tayari zimekwishaandaa miundombinu ya Soko la Madini. Tume ya Madini iko katika taratibu za kuliwezesha soko hilo kwa vifaa vya kitaalam ikiwamo mashine ya XRF na Geomological Tool Kit kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kitaalam.
Pia kufuatia uchimbaji mwingi kuwa wa madini yasiyoweza kuuzwa sokoni mfano Mkaa wa Mawe na Madini Ujenzi, elimu imeendelea kutolewa kwa wachimbaji wenye leseni za uchimbaji wa madini yanayoweza kuuzwa sokoni kufanya uchimbaji endelevu utakaovutia wanunuzi wa madini kutoka maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi na maeneo ya mipakani Ofisi ya Madini imeendelee kushirikiana na vyombo vya Usalama kuweza kuwaelekeza watu wote kutoka nchi jirani kuingia na madini yao na kuyauza kwenye soko la madini.
Aina za madini yanayopatikana katika Mkoa wa Rukwa
Hadi kufikia tarehe 19 Februari, 2018 Mkoa ulikuwa na jumla ya watafiti 24 wenye leseni (Prospecting Licences) za kutafuta madini na wachimbaji wadogo 191 wenye leseni za uchimbaji wa madini (Primary Mining Licences) kwa vikundi au mmoja mmoja.
Aina za madini yanayopatikana katika Mkoa wa Rukwa
Na. |
Madini |
Yanakopatikana |
Halmashauri |
1
|
Copper
|
Kasanga na Kapapa
Ifumwe |
Kalambo
Nkasi |
2
|
Zinc
|
Kasanga na Kirando katika mwambao wa Ziwa Tanganyika
|
Kalambo na Nkasi.
|
3
|
Titanium and Zirconium
|
Ntemba na Mkwamba
|
Nkasi
|
4
|
Emerald
|
Mponda
|
Manispaa ya Sumbawanga
|
5
|
Aquamarine
|
Mlombo kilometa chache mashariki mwa bwawa la Kwela
|
Wilaya ya Sumbawanga
|
6
|
Burma Ruby
|
Katuka, Chala na Kantawa
|
Wilaya Sumbawanga, Nkasi
|
7
|
Zircon
|
Nzombo kijiji cha Matala.
|
Nkasi
|
8
|
Piezoelectric Quartz
|
Kijiji cha Matala
|
Nkasi
|
9
|
Moonstone
|
Mkombe Kaskazini mwa kijiji cha Kabwe mwambao wa ZiwaTanganyika
|
Nkasi
|
10
|
Green Tour- maline
|
Chala, Swaila, Lyele na Tambaruka
|
Nkasi
|
11
|
Garnets
|
Kantawa, Chala
|
Nkasi
|
12
|
Amethyst
|
Kasu na Lyazumbi
|
Nkasi
|
13
|
Coal
|
Muze, Namwele na Nkomolo
|
Wilaya ya Sumbawanga na Nkasi
Manispaa ya Sumbawanga |
14
|
Kaolin
|
Kufuata Barabara ya Sumbawanga hadi Kasanga
|
Sumbawanga na Kalambo
|
15
|
Limonite
|
Mbuga/ Namwele
|
Manispaa ya Sumbawanga
|
17
|
Kyanite
|
Kizi, Chala na Tambaluka
|
Nkasi
|
18
|
Helium gas
|
Bonde la Ziwa Rukwa
|
|
Chanzo: Ofisi ya madini ya Kanda (Mpanda)
Kwa mujibu wa takwimu kutoka Ofisi ya Madini Kanda yetu ya Magharibi, madini yanayochimbwa zaidi katika mkoa wa Rukwa ni makaa ya mawe na Madini ya ujenzi. Kiasi cha makaa ya mawe yaliyochimbwa mwaka 2007–2008 eneo la Namwele lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ni tani 3,692.7 yenye thamani ya Shilingi 107, 669,167. Makaa hayo yaliyochimbwa na Kampuni ya Upendo Group Limited yaliuzwa kwenye kiwanda cha Mbeya Cement.
Uwepo wa gesi ya Helium katika Mkoa
Taarifa ya tarehe 19 Februari, 2018 kutoka Ofisi ya Madini ya Kanda-Mpanda inaeleza kuwa mwezi Mei, 2016 Kampuni ya Helium One Ltd. inayomiliki leseni 8 za utafutaji wa Gesi ya Helium Mkoani Rukwa kupitia Kampuni zake tanzu za Togota (T) Limited, Njozi (T) Limited na Stahamili (T) Limited iligundua uwepo wa Gesi ya Helium Mkoani Rukwa. Kwa mujibu wa makadirio yaliyofanyika, inaonesha kwamba Gesi hii ipo kwa kiasi kisichopungua futi za ujazo Bilioni hamsini na nne (54cf).
Kampuni inatarajia kuanza kufanya uchorongaji kabla ya mwezi Julai mwaka huu (2018) kwa lengo la kupata kiasi halisi kilichopo katika eneo hilo ili uchimbaji uanze rasmi. Maeneo ilipogundulika Gesi hii ni Kusini Mashariki mwa Ziwa Rukwa eneo la Gua na Mto Lwiche kwa upande wa Magharibi mwa Ziwa Rukwa. Upatikanaji huu wa Gesi ya Helium utachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Mkoa wa Rukwa na Nchi kwa ujumla.
Ombi kwa Wawekezaji
Kutokana na fursa hizo za madini mbalimbali kuwepo katika Mkoa hii inamaanisha uhitaji wa huduma mbalimbali kwa watumishi wa migodi hii kama vile shule, vyakula, hoteli za kisasa, kumbi za mikutano, n.k
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 1 Barabara ya Mkoani
Sanduku la barua: Box 128 Sumbawanga, 55180 RUKWA
Simu: 025 280 2137
Simu: 0739862632
barua pepe: ras@rukwa.go.tz
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa