Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (Ewura) imetoa mafunzo kwa wafanyabiashara wa mafuta na vilainishi Mkoani Rukwa ambapo imewataka wafanya biashara hao kufuata sharia, kanuni na taratibu zilizowekwa kwa bidhaa hizo.
Katika mafunzo hayo mkurugenzi wa idara ya Petroli kutoka Ewura GODWIN SAMWEL amesema kuwa wameamua kutoa mafunzo hayo nchi nzima ili kuondokana na hali ya uharibifu wa magari ya wananchi kwakuwa vilainishi vingine havijathibitishwa kutumika nchini na vinaingizwa kinyemela.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa mamlaka hiyo, imejipanga vyema pamoja na kushirikiana na jeshi la polisi ili kuhakikisha kuwa vilainishi ambavyo havijathibitishwa kutumika nchini vinakamatwa, kutaifishwa na wafanyabiashara wanaohusika na biashara hiyo wanakamatwa kisha kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Hata hivyo baadhi ya wafanyabiashara wamepongeza kupewa mafunzo hayo ambapo wameitaka Ewura kuendelea kutoa mafunzo hayo mara kwa mara ili kujiepusha na majanga mbalimbali.
Mbali na mafunzo hayo kutolew Mkoani Rukwa lakini bado mwitikio wa wafanyabiashara wa mafuta umekuwa sio wa kuridhisha ukilinganisha na vituo vya mafuta vilivyopo mkoani humo.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa