WAZIRI MKUU,Kassim Majaliwa amezindua Bandari ya Kabwe uliyojengwa na kampuni yaKitanzania ya Sumry’s Enterprises kwa thamani ya sh. bilioni saba.
Ujenzi huo wa Bandari ya Kabwe yenye eneo la ukubwa wa mitaza mraba 10,864 unalenga kuongeza tija katika shughuli za bandari kwenyemwambao wa Ziwa Tanganyika na kupanua fursa za kibiashara.
Waziri Mkuu amezindua bandari hiyo leo (Jumapili, Julai 05,2020) wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Rukwa. Bandari hiyoimenjengwa Kata ya Kabwe, wilayani Nkasi, Rukwa.
Waziri Mkuu ameipongeza kampuni ya Sumry’sEnterprises kwa kujenga vizuri mradi huo . “Rais wetu Dkt. Magufuli amesemaWatanzania tunaweza na huyo mkandarasi amedhirisha hilo.”
“Hizi ni jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tanoinayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuhakikisha maendeleleoyanawafikia wananchi wote bila ya ubaguzi.”
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wananchiwashirikiane na Serikali katika kulinda miundombinu ya mradi huo iliiweze kudumu.
“Hatuna historia mbaya hapa, endeleeni kudumisha uaminifuna uadilifu ili bandari hii iwe ni mahali salama kwa abiria na mizigo. Bandarihii itaongeza fursa kibiashara kati yetu na nchi jirani.”
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlakaya Bandari Tanzania (TPA) Dkt. Baraka Mdima amesema mradi huo utakuwa chachu yakukuza uchumi na kuboresha usafiri.
“Mradi huu wa bandari utaboresha usafiri wa majini kwawananchi waishio kandokando ya Ziwa Tanganyika hususani wilaya ya Nkasi nakatika kata ya Kabwe na vijiji vinavyoizunguka.”
Amesema mradi umehusisha ujenzi wa gati la kupaki melilenye uwezo wa kuhudumia meli kubwa za kubeba abiria na mizigo zenye urefu hadimita 75 na miundombinu mingine ya bandari kama jengo la kupumzikia abiria,majengo ya ofisi, nyumba za kuishi watumishi na eneo la mgahawa.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa