• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

MIRADI YA BILIONI 56.7 YAKAGULIWA KALAMBO

imewekwa Tar: September 25th, 2023

Miradi 11 yenye thamani shilingi Bilioni 56.7 imekaguliwa na Kamati ya Siasa ya Mkoa ya Chama cha Mapinduzi Wilayani Kalambo.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Rukwa Bi Silafu Jumbe Maufi imekagua ujenzi wa Miradi 02 ya Maji katika Vijiji vya Singiwe na Kalaela yenye thamani ya  Shilingi Bilioni 16, Ujenzi wa  barabara kwa kiwango cha lami barabara ya Matai - Kasesya na Matai - Kisungamile  yenye thamani ya Shilingi Bilioni 37.8.

Miradi mingine ni mradi wa ujenzi wa miundombinu ya Hospitali ya Wilaya ya Kalambo ( wodi ya wazazi) yenye thamani ya shilingi milioni 250,  Ujenzi wa Vituo viwili vya Afya vya Samazi na Legezamwendo vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.2, mradi wa ujenzi wa shule  mbili  mpya za Msingi za Matai  na Kalepula zenye thamani ya shilingi Bilioni 1.2.

Kamati hiyo imekagua pia  mradi wa ujenzi wa vyumba nane vya madarasa  Shule ya Sekondari Mambwe  yenye thamani ya Shilingi Milioni 160 na mradi wa skimu ya umwagiliaji wenye thamani ya shilingi milioni 202.

Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Rukwa imempongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi hiyo.

Kamati ya Siasa ya Mkoa  imeipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, RUWASA, TARURA na TANROADS kwa usimamizi mzuri wa miradi.

Aidha  Kamati hiyo imewataka wakandarasi  kuhakikisha miradi ya maendeleo  wanayoitekeleza kuikamilisha kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa ili kutimiza malengo ya Serikali kuboresha na kusogeza huduma karibu na wananchi.

Matangazo

  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2025 April 15, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA NNE 2024 January 04, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONGORO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

    May 05, 2025
  • JAMII YAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUWAHUDUMIA WAZEE

    March 19, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI MKOA WA RUKWA

    January 09, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA MSIMU WA SIKUKUU WA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI RUKWA

    December 31, 2024
  • Angalia Zote

Video

LIVE- WAZIRI MCHENGERWA ANATAO TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Mfumo wa Kutuma, Kupokea na kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa