• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Miradi ya shule ya Shilingi Bilioni 1.15 iliyoshindikana kumalizika yamuibua RC Wangabo.

imewekwa Tar: December 27th, 2020

Serikali kupitia miradi yake ya Afya na Usafi wa Mazingira (SWASH) Pamoja na mradi wa Lipa kulingana na Matokeo (EP4R) imeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa jumla ya kiasi cha Shilingi 1,152,557,008.77/= kwaajili ya kutekeleza ujenzi wa madarasa 18, matundu ya vyoo 178, mabweni mawili kwa shule za Msingi na Sekondari fedha ambayo halmashauri hiyo ilipatiwa tangu mwezi Juni mwaka 2020 lakini hadi kufikia mwezi Disemba 2020 ujezni wake haujafikia hata asilimia 50 ya ukamilishaji.

Kutokana na kuchelewa kwa utekelezaji wa miradi hiyo Mkuu wa mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo amekemea uzembe unaofanywa na viongozi wa halmashauri hiyo huku akisikitishwa na kitendo cha Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Msongela Palela kuchukua ruhusa ya kuondoka nje ya mkoani huo huku katika halmashauri yake kukikosekana madarasa saba kwaajili ya wanafunzi 254 waliokosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza katika halmashauri hiyo.

Mbali na fedha za miradi hiyo wananchi wa Kata ya Matai kwa kushirikiana na halmshauri wameanza ujenzi wa vyumba vya madarasa manne katika shule ya Sekondari Matai ambavyo vinatakiwa kukamilika kabla ya tarehe 28.2.2021 kwaajili ya kuwapokea wanafunzi waliokosa nafasi katika awamu ya kwanza ya uchaguzi wa wananfunzi hao wilayani humo.

Akizungumza katika ziara yake ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya shule za Msingi za Sekondari katika Halmshauri hiyo wakati alipokuwa katika Shule ya Sekondari Matai inayotekeleza ujenzi wa madarasa sab ana mabweni mawili Mh. Wangabo alisema kuwa amekosa Imani na utendaji kazi wa halmashauri hiyo baada ya kuona miradi inayogharamiwa na serikali kutomalizika kwa wakati huku miradi inayotekelezwa kwa kushirikiana gharama na wananchi kutokuwa na dalili ya kumalizika.

“Miezi sita lakini watu wanafanya utekelezaji kwa 42% sasa mimi inanipa mashaka,huku tu ambako kuna fedha ujenzi haujakamilika kwa miezi sita, je hukuambako tunaanza msingi nahakuna fedha ni juhudi za wananchi tutakamilisha baada ya muda gani? Ninayasema haya kwa uchungu mkubwa kwasababu angalau mngenitia Imani kwamba ile fedha ya serikali iliyopokelewa Shilingi milioni 756 zilikwisha kamilika na miundombinu yote inaonekana na iko vizuri kwa ubora wake,lakini hakuna tuko  42% hatujamaliza na tuna mzigo mkubwa wa haya madarasa tuko kwenye msingi, Imani kwangu itatoka wapi kwamba huu ujenzi tutaukamilisha ndani ya iezi miwili, ndugu wanachi tutafika?” Alihoji.

Aidha, Aliutaka uongozi wa Halmashauri hiyo kufanya kazi ya ziada ili kutekeleza maagizo ya serikali ili kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza wanaendelea na masomo yao kama ilivyoelekezwa.

“Niwaagize uongozi wa Wilaya hususani Mkurugenzi ambaye najua hapa hayupo, watu wameambiwa wasisafirisafiri yeye anasafirisafiri, watu wasiende likizo yeye hayupo hapa, miundombinu haipo, sasa tutafika namna hii, nitakuja tena baada ya wiki mbili kuona hatua ambayo tumeifikia,” Alisema.

Wakati akitoa taarifa ya Wilaya hiyo Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Carolius Misungwi alieleza mikakati mbalimbali iliyowekwa na Wilaya ili kufanikisha azma ya serikali katika kuhakikisha wanamaliza ujenzi wa madarasa hayo na wanafunzi hao kuendelea na masomo ifikapo mwezi Februari 2021.

“Wilaya imeweka mikakati mbalimbali ikiwemo kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari za Kalambo, Matai, Msanzi, Mwazye na Mambwe. Vyumba sita vya madarasa vya Shule ya Sekondari Wasichana matai vitatumika kwa muda wakati ujenzi wa vyumba 7 unakamilika katika shule ya Sekondari Matai,” Alisema.

Serikali kupitia miradi yake hiyo imetoa Shilingi 756,278,504.77/= kwaajili ya kujenga vyumba vya madarasa 18 wilayani Kalambo ambapo vyumba  15 ni vyashule ya Msingi na vyumba 3 vya Shule ya Sekondari Matai ambavyo havijakamilika na Kiasi cha Shilingi 229,678,504/= kwaajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo 178 katika shule za msingi na Shilingi 6,600,000/= kwaajili ya ujenzi wa matundu sita ya vyoo katika Shule za sekondari na kiasi cha Shilingi 160 kwaajili ya ujenzi wa Mabweni mawili katika Shule ya Sekondari Matai ambayo nayo hayajakamilika na hivyo kufanya miundombinu yote kuwa katika silimia 42 ya utekelezaji wake.

Matangazo

  • HOTUBA YA BAJETI YA TAMISEMI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024 May 05, 2023
  • Bei ya Mbolea za Rukuzu kwa Wakulima August 31, 2022
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi April 20, 2022
  • Hotuba ya Bajeti ya WN -OR TAMISEMI 2022/23 April 20, 2022
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WAWEKEZAJI KUTOKA ZAMBIA WAVUTIWA NA BANDARI MKOANI RUKWA

    May 28, 2023
  • MRADI WA MAJI WAZINDULIWA KISA

    May 15, 2023
  • ZAHANATI YA MPONA HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA YAZINDULIWA

    May 15, 2023
  • UPENDO, MAADILI NA FAMILIA IMARA MUAROBAINI WA UKATILI WA KIJINSIA

    May 15, 2023
  • Angalia Zote

Video

Serikali Kuimarisha mahusiano na Sekta Binafsi
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Kilio cha Wananchi kinasikilizwa
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 1 Barabara ya Mkoani

    Sanduku la barua: Box 128 Sumbawanga, 55180 RUKWA

    Simu: 025 280 2137

    Simu: 0739862632

    barua pepe: ras@rukwa.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa