Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 ukiongozwa na Ndugu Abdalla Shaib Kaim Leo Agosti 29 2023 umezindua miradi 03, umeweka jiwe la msingi Mradi 01na umekagua mradi 01 katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.4
Miradi iliyozindundiliwa ni miradi wa Maji- Lyazumbi wenye thamani ya Shilingi Milioni 331,Mradi endelevu wa maji na usafi wa mazingirana maboresho ya wodi ya wazazi katika Zahanati ya Paramawe wenye thamani ya Shilingi Milioni 65 , mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa 10 shule ya Sekondari Kirando yenye thamani ya shilingi Milioni 201, umeweka jiwe la msingi daraja la Kivunja lenye Thamani ya Shilingi Milioni Bilioni 1.6 na kukagua na kutembelea shuguli za vijana.
Akiongea na hadhara ya wananchi Wilayani Nkasi katika Kata ya Kirando katika viwanja vya Polisi, Ndugu Abdala Shaibu Kaim ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, RUWASA na TARURA kwa kuwa na miradi mizuri ambayo inazingatia ubora pamoja na thamani ya fedha huku akisisitiza kuhakikisha maelekezo yote yaliyotolewa yanafanyiwa kazi.
Akiwa katika chanzo cha Maji Bwawa la Mfili ameridhishwa na kuwapongeza wananchi wa Wilaya ya Nkasi kwa namna ambavyo wametekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 isemayo”Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumba Haina Uchumi wa Taifa”.
Pia amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Taasisi ya Kupambana na Kuzia Rushwa nchini kwa kutoa ushahidi Mahakamani ili kuunga juhudi za Serikali katika kutokomeza Rushwa nchini ili kuweza kuteleza kwa vitendo ujumbe wa Mwenge 2023 unaosema “ Kuzuia Rushwa ni Jukumu Lako, Langu tutimize Wajibu wetu.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa