Mwenge wa Uhuru 2024 umepokelewa Mkoani Rukwa leo tarehe 05 Septemba 2024 ukitokea Mkoani Songwe. Mwenge wa uhuru utakimbizwa Mkoani Rukwa kwa siku 4 huku ukitarajia kutembelea, kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo 32.
Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ameeleza hayo mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg. Godfrey Eliakimu Mnzava wakati akiupokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Songwe.
Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Rukwa utakimbizwa umbali wa Km 520 katika Wilaya za Sumbawanga, Wilaya ya Kalambo na Wilaya ya Nkasi.
Mwenge wa Uhuru umeanza kukimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ambapo miradi 4 imekaguliwa, miradi 3 imewekewa jiwe msingi na miradi 3 imezinduliwa. Miradi hiyo ina thamani ya shilingi bilioni 3.9.
Akizungumza katika vipindi tofauti Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg. Godfrey Mnzava amezitaka taasisi zote za Umma kufanya manunuzi yote katika mfumo wa NeST.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa