RC MAKONGORO, ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA 33 YA BARABARA YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 7
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere ameshuhudia utiaji saini wa mikataba 33 ya matengenezo ya barabara kwa Mwaka 2024/2025 yenye thamani ya shilingi bilioni 7.7.
Hafla hiyo ya utiaji saini wa mikataba kati ya TARURA na Wakandarasi imefanyika leo Agosti 12, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Akizungumza katika hafla hiyo Mheshimiwa Makongoro amegusia juu ya uharibifu mkubwa wa miundombinu uliofanywa na mvua za msimu uliopita na kuwataka wananchi kutoharibu mazingira ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha Mkuu wa Mkoa ameishukuru Serikali kwa ongezeko la bajeti ya barabara kwa Mkoa wa Rukwa kutoka Shilingi bilioni 5.19 Mwaka 2020/2021 hadi Shilingi bilioni 11.84 Mwaka 2024/2025 na kuitaka TARURA kusimamia kwa ukaribu kazi zote ili zikamilike kwa wakati na ubora huku akitaka Wakuu wa Wilaya na TAKUKURU kupatiwa nakala za Mikataba hiyo ili kusaidia usimamizi.
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Makongoro ameshauri kufanyika hafla za kusaini mikataba ili kuweka mazingira ya uwazi na uwajibikaji.

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa