• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

RC Rukwa aitahadharisha TARURA kutorudia makosa ya Halmashauri.

imewekwa Tar: October 11th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameutahadharisha Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini kutorudia makosa yaliyokuwa yanafanywa na Halmashauri kabla ya wakala huo kuanzishwa.

Amesema kuwa matumizi mabaya ya fedha za barabara pamoja na barabara hizo kujengwa chini ya viwango na kuisababishia serikali hasara ya kufanya matengenezo ya mara kwa mara ni miongoni mwa changamoto ambazo serikali imeamua kuzitafutia ufumbuzi kwa kuanzisha Wakala huo.

“Ukiitwa Injinia na kazi yako iendane na cheo chako, sio unafanya kazi mpaka hata sisi ambao hatuna ujuzi huo tukiona tunasema hii ipo chini ya kiwango, na hapo mwanzo serikali ilikuwa inaelekeza pesa nyingi sana kwenye barabara lakini kiuhalisia barabara hazipo na muda mwingine mvua zinataka kuanza ndio utaona mkandarasi anaingia barabarani kwenda kutengeneza barabara,” Mh. Zelote alifafanua.

Ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha kwanza cha bodi ya barabara kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Amesisitiza kuwa kwa kuimarisha sekta ya barabara vijijini ndio miongoni mwa hatua za kuuendea uchumi wa Viwanda ambao ndio kipaumbele cha serikali ya wamu ya tano inayoongozwa na Mh. Dk. John Pombe Magufuli.

Hivyo ametoa wito kwa wakala huo kuhakikisha wanafanya kazi yao kwa uadilifu na kuhakikisha mabadiliko yanaonekana na kuwaasa kuacha kufanya kazi kwa mazoea na hatimae kurudisha nyuma azma ya serikali ya awamu ya tano. 

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAILI October 24, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA - MAPOKEZI YA FEDHA KIASI CHA SHILINGI BILIONI 3.8 KWA AJILI YA SEKTA YA AFYA October 05, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI- RUKWA September 27, 2023
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 13, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MAKONGORO AWATAKA WADAU KUILIPA TEMESA KWA WAKATI

    November 21, 2023
  • MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA; WANAFUNZI RUKWA KUGAWIWA VYANDARUA

    October 19, 2023
  • MAKONGORO ATAKA MIRADI IKAMILIKE KABLA YA OKTOBA 30, 2023.

    October 18, 2023
  • KIWANJA CHA NDEGE SUMBAWANGA KUKAMILIKA MACHI 2025

    October 02, 2023
  • Angalia Zote

Video

Serikali Kuimarisha mahusiano na Sekta Binafsi
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Kilio cha Wananchi kinasikilizwa
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 1 Barabara ya Mkoani

    Sanduku la barua: Box 128 Sumbawanga, 55180 RUKWA

    Simu: 025 280 2137

    Simu: 0735019734

    barua pepe: ras@rukwa.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa