Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka watanzania kutumia unga wa Energy Sembe pamoja na maji ya Dew Drop yanayozalishwa Mkoani Rukwa na kusambazwa zaidi ya Miko saba nchini ili kuona ubora wa bidhaa zinazotengenezwa katika Mkoa wa Rukwa.
Ameyasema hayo alipotembelea kiwanda cha Unga cha Energy Sembe pamoja na Kiwanda cha Maji ya Dew Drop vyote vinamilikiwa na mwekezaji mzawa wa Mkoa wa Rukwa Aziz Sudi katika ziara ya siku moja aliyoifanya katika Manispaa ya Sumbawanga ili kujionea maendeleo ya Viwanfda mablimbali pamoja na miradi ya maendeleo inyaotekelezwa na manispaa.
“Nitoe rai kwa wananchi wote Tanzania watumie Energy Sembe kutoka Rukwa ni bora yenye viwangona kingine ni hiki kiwanda cha Dew Drop ambacho kinatengeneza maji yenye kiwango cha juu sana na yanasambazwa zaidi ya mikoa saba nchini, tutumie maji haya, tujivunie viwanda vyetu vya hapa hasa hivi ambavyo vinazalishwa na wazawa wenyewe,” Alisema.
Kwa upande wake Mwekezaji huyo Aziz Sudi amesema kuwa maji ya Dew Drop ni maji yasiyotumia kemikali ya aina yoyote na kuwa ni maji halisi na kuongeza kuwa ni tofauti na maji mengine yanayowekwa kitu kinachofanana na “water guard” jambo linalobadilisha ladha ya maji.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa