Mkoa wa Rukwa umepokea madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Kambi maalum ya matibabu ya moyo imeanza rasmi tarehe 20 Mei 2024 na itadumu hadi tarehe 24 Mei 2024, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa iliyoko Sumbawanga.
Akizungumza katika zoezi hilo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa JKCI Dkt Saleh Hamisi Mwinchete amesema lengo la kambi hiyo ni kutoa huduma za kimatibabu ya magonjwa ya moyo, kutoa ushauri na elimu kwa wananchi namna ya kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza na kutoa mafunzo na kubadilishana uzoefu na madaktari wa magonjwa ya moyo wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ili waendelee kutoa huduma bora zaidi kwa wagonjwa.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa