Mkoa wa Rukwa umepokea madaktari bingwa 20 kwa ajili ya kuwahudumia wakazi wa Mkoa wa Rukwa. Kundi hilo la madaktari linajumuisha madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake, watoto, magonjwa ya ndani, usingizi na upasuaji.
Huduma za madaktari bingwa hao zitatolewa kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 13 Mei, 2024 hadi tarehe 17 Mei, 2024 katika hospitali za Wilaya zote za Mkoa wa Rukwa. Hospitali hizo ni pamoja na Hospitali ya Manispaa ya Sumbawanga iliyoko Isofu, Hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga iliyoko Mtowisa, Hospitali ya Wilaya ya Kalambo iliyoko Matai na Hospitali ya Wilaya ya Nkasi iliyoko Namanyere
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Ibrahim Issack Mwita ameishukuru Serikali kwa kusogeza huduma mikoani kwa kuwa inawapunguzia wagonjwa gharama kubwa za kufuata huduma za kibingwa.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa