Katika Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani mkoani Rukwa Katibu wa chama cha wafanyakazi Mkoani Rukwa amewatakata viongozi wa vyama vya wafanyakazi kuhakikisha wanatoa mafundisho yanayolenga kuwaamsha wanachama juu ya mabadiliko ya sheria yanayojitokeza mara mara ili kuwa na uelewa wa haki zao.
“Natoa wito kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi pamoja na kuwaomba maafisa kazi kuwa na tabia ya kusoma sheria makazini na kuwafundisha wanachama wao, kwani kiumekuwa na mabadiliko ya sheria ambazo wafanyakazi hawazifahamu hivyo wanahitaji kukumbushwa,”Alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa amewataka waajiri wote kuruhusu mabaraza ya kazi kufanyika kwa wakati na kuhakikisha wafanyakazi bora wanaongezewa kiwango cha zawadi ili kuongeza ushindaji wa utendaji kazi na hatimae kuinua uchumi wa Mkoa na wa Nchi kwa ujumla.
“Zawadi wanazopatiwa wafanyakazi bora ziongezwe, na wanaotangazwa kupewa zawadi wapewe kwa wakati ili wale ambao hawakupata mwaka huu, mwakani wajitahidi na hatimae kuleta ushindaji katika kutimiza majukumu yetu ya kila siku,” Alisema.
Pia alipongeza utaratibu wa chama cha wafanyakazi kuzifanya sherehe hizo kwa mzunguko katika kila Wilaya huku akieleza kuwa mwaka 2016, ilifanyika Wilaya ya Kalambo, mwaka 2017 ilifanyika Wilaya ya Nkasi na mwaka huu kufanyikia Wilaya ya Sumbawanga.huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa 'Kuunganishwa kwa mifuko ya jamii kulenge kuboresha mafao ya wafanyakazi'
Hayo yalijitokeza katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani inayosheherekewa kila ifikapo tarehe 1 mwezi wa 5 ya kila mwaka ambapo mwaka huu ilifanyikia katika viwanja vya Mandela, katika Manispaa ya Sumbawanga.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa