WAGONJWA 957 WAPATIWA HUDUMA ZA KIBINGWA MKOANI RUKWA
Wagonjwa 957 wamepatiwa huduma za kibingwa Mkoani Rukwa.
Akitoa taarifa ya hali ya huduma leo tarehe 17 Mei 2024, Dkt Budodi ambaye ni mratibu wa kambi ya huduma za kibingwa za matibabu amemweleza Mheshimiwa Charles Makongoro Nyerere, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, kuwa jumla ya wanawake 694 na wanaume 353 wamepatiwa huduma za kibingwa za magonjwa mbalimbali.
Mheshimiwa Makongoro amepokea taarifa hiyo alipotembelea Hospitali ya Manispaa ya Sumbawanga kujionea hali ya utoaji huduma za kibingwa Mkoani Rukwa.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo Mheshimiwa Mkuu Mkoa wa Rukwa ameishukuru na kuipongeza Serikali kwa ubunifu uliosaidia kupunguza gharama za huduma na umbali kwa wagonjwa wa Mkoa wa Rukwa.

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa