Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo amewagiza wakuu wa wilaya pamoja na viongozi wote wa Halmashauri kusimamia kwa ukaribu zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na kuahakikisha kila mwananchi anashiriki na kujiorozesha kwenye daftari hilo.
Akiwa katika ziara ya ukaguzi wa vituo vya kuandikisha wapiga kura wilayani Kalambo ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika 24 Novemba 2019, Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amesema mpaka sasa wananchi 259,783.
“Mpaka sasa waliojiandikisha kupiga kura kwa mkoa wa Rukwa ni 259,783 kati ya waandikishwaji ambao tunawakadiria kufikia 568,162 Wilaya ya Kalambo mpaka sasa wamejiandikisha kwa asilimia 36 na Nkasi asilimia 35, Manispaa ya Sumbawanga ni asilimia 37 na halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga wanaongoza wakiwa na asilimia 70, na hii inafanya kwa mkoa kuwa na asilimia 47.5 mpaka sasa,”
Aidha amewataka wakuu wawilaya kusimamia kwa ukaribu zoezi hilo ili liweze kwenda vizuri.
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Mh.Julieth Binyura, amesema mawakala wa vyama vya siasa wanalojukumu la kuwasaidia waandikishaji kuwatambua wageni ili wasijiandikishe kwenye daftali la wapiga kura kwani hawana haki hiyo kisheria.
“Nawaasa wananchi wote tuweze kujitokeza tujiandikishe ili tuweze kupiga kura, kura itakayopigwa tarehe 24 mwezi wa 11, 2019 wananchi wote tuweze kupiga kura na tuwachague viongozi ambao wanafaa kabisa, katika kutatua matatizo yetu katika kuendeleza nchi yetu na wilaya yetu ya Kalambo kwa ujumla na watumishi wetu wa serikali pia wajiandikishe kwaajili ya kupiga kura tuchague viongozi wetu wa vijiji na vitongoji,”Alisema.
Waziri wa Ofisi uya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Suleiman Jafo ameongeza siku tatu kwa wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura ili kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa mwezi Novemba, 24, 2019, zoezi ambalo lilitegemewa kumalizika tarehe 14 na hivyo sasa zoezi hilo linategemewa kumalizika tarehe 17, 10, 2019.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa