• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Rukwa Region
Rukwa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Rukwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Sumbawanga
    • Wilaya ya Nkasi
    • Wilaya ya Kalambo
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Sumbawanga
    • H/Wilaya ya Nkasi
    • H/Wilaya ya Kalambo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Miundombinu ya Rukwa
  • Huduma zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Livestocks
    • Huduma za Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Huduma za Kisheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Fedha
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
    • Waliofaulu na Waliochaguliwa Shule

Waziri Mkuu Aanza Ziara Rukwa

imewekwa Tar: December 14th, 2022

MAJALIWA : HALMASHAURI TUMIENI FEDHA ZA NDANI KUKAMILISHA MIRADI

Na. OMM Rukwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Rukwa ambapo ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Paramawe na hospitali ya Wilaya iliyopo Wilayani ya Nkasi.

Akiwa katika Shule ya Sekondari Paramawe leo (Desemba 14,2022) inayojengwa kupitia mradi wa SEQUIP ambapo ameweka jiwe la msingi la mradi huo uliogharimu Shilingi Milioni 470 kujenga vyumba nane vya madarasa,maabara,maktaba na matundu ya vyoo.

Akizungumza baada ya kukagua ujenzi huo, Waziri Mkuu amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo Rashid Mchatta kumsimamia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi William Mwakalambile ili ahakikishe anakamilisha maeneo ya ujenzi wa shule hiyo kwa kutumia mapato ya ndani.

“Milioni 470 zimetumika na mmetumia zingine za halmashauri lakini miundombinu bado. Nataka shule hii ikamilike na Januari 2023 wanafunzi waingie” Alisema Majaliwa

Kuhusu ujenzi wa hospitali ya Wilaya Nkasi, Waziri Mkuu aliewaeleza wananchi kuwa serikali itaendelea kukamilisha miradi yote ya afya ikiwemo kuhahikisha vifaa tiba vinapatikana kwa ajili ya wananchi kupata huduma.

Aidha, Waziri Mkuu amemwagiza Naibu Katibu Mkuu  Tamisemi -Afya kukutana na uongozi wa halmashauri ya Nkasi ili kujua kwanini mradi ya ujenzi wa majengo saba ya hospitali ya wilaya haujaanza wakati tayari fedha zilikwishatolewa na serikali.

“Naibu Katibu Mkuu Tamisemi urudi hapa Nkasi kesho kufuatilia kwanini majengo saba hayajaanza wakati fedha ipo” aliagiza Waziri Mkuu Majaliwa.

Katika hatua nyingine Majaliwa ameagiza Mkuu wa Mkoa huo na Katibu Tawala wa Mkoa kuitisha kikao cha mawakala wa mbolea mapema iwezekanavyo ili kuhakikisha wakulima wanapata pemebejeo hiyo muhimu kwa kuwa serikali imekwisha toa fedha za ruzuku .

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga alisema mkoa unaendelea na usimamizi wa shughuli za maendeleo na kuwa wananchi watapata huduma stahiki.

Waziri Mkuu kesho ataendelea na ziara yake kwenye wilaya za Kalambo na Sumbawanga.

Mwisho.

Matangazo

  • Bei ya Mbolea za Rukuzu kwa Wakulima August 31, 2022
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi April 20, 2022
  • Hotuba ya Bajeti ya WN -OR TAMISEMI 2022/23 April 20, 2022
  • Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) October 09, 2018
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • JAMII ISHIRIKIANE NA WALIMU KUKUZA TAALUMA

    February 16, 2023
  • Kampeni Upandaji Miti

    February 07, 2023
  • TASAF

    February 05, 2023
  • RAS Mchatta akagua miradi

    January 26, 2023
  • Angalia Zote

Video

Serikali Kuimarisha mahusiano na Sekta Binafsi
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miundombinu ya Rukwa
  • Uvuvi
  • Mikakati ya Mkoa
  • Industries
  • Madini
  • Speeches
  • Huduma za Kilimo
  • Regional History
  • Hotuba

Viunganishi Linganifu

  • Pakua Salaryslip yako hapa
  • Idara ya Takwimu (NBS)
  • Kilio cha Wananchi kinasikilizwa
  • Watumishi portal
  • Tafuta ajira Serikalini
  • Pata kila kitu kutoka serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Wapitiaji

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 1 Barabara ya Mkoani

    Sanduku la barua: Box 128 Sumbawanga, 55180 RUKWA

    Simu: 025 280 2137

    Simu: 0739862632

    barua pepe: ras@rukwa.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa