Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso (Mb) anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili kwenye wilaya za Sumbawanga, Kalambo na Nkasi kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maji Vijijini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (15.12.2021) na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Denis Bandisa imesema Waziri Aweso ataanza ziara hiyo tarehe 17 na 18 mwezi huu ambapo atazindua miradi mitatu ya maji kijiji cha Kizungu , Sopa na Kitete wilaya ya Kalambo.
Katika siku ya pili ya ziara yake atakagua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maji ya kijiji cha Kirando na Kisura wilaya ya Nkasi pamoja na kuzungumzia na wananchi kwenye maeneo ya miradi.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Rukwa Mhandisi Pius Boaz alisema maandalizi ya ziara hiyo yamekamilika na kuwa wananchi wajitokeze kwenye maeneo ya miradi ili wamsikilize Waziri.
Mwisho.
Hakimiliki © 2017 Mkoa wa Rukwa. Haki Zote Zimehifadhiwa